1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya Umoja wa mataifa ya mshikamano na Wapalestina

29 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CHL5

Leo ni siku ya Umoja wa mataifa ya mshikamano na Wapalestina.

Tarehe 29 Novemba 1947, umoja wa mataifa uliandaa mpango kwa ajili ya Wapalestina, kuhusiana na mgogoro kati ya Waarabu na Wayahudi juu ya Palestina iliokua chini ya mamlaka ya Uingereza. Mpango huo uliigawa Palestina pande mbili, sehemu moja kwa wayahudi na nyengine ikapendekezwa kuwa taifa la Palestina huku ikipendekezwa sehemu kubwa ya Jerusalem iwe katika usimamizi wa kimataifa. Mpango huo ndiyo uliozusha vita 1948 baina ya waisraili na waarabu-vita vya kwanza vya Palestina.

Kuna sababu ya msingi kwa umoja wa mataifa kuichukulia tarehe 29 Novemba kuwa siku ya mshikamano na umma wa wapalestina. “Wapalestina ni umma usiyo na bahati duniani”, ni maneno ya mwandishi habari wa Kiisraili Shlomi Eldar katika kitabu chake kuhusu hujuma za miaka iliopita katika ukanda wa Gaza.

Pengine mwandishi huyo wa habari wa televisheni haujuwi umma mwengine unaotaabika zaidi ya wapalestina. Kwa hakika kuna wengi wasio na bahati na wenye kukandamizwa.Kuna wanaokandamizwa na serikali zao wenyewe, mfano Korea kaskazini na Zimbabwe.

Ndiyo kuna umma ambao umekandamizwa na kuangamizwa kwa taratibu za mpangilio za tawala na madikteta dhidi ya watu wao wenyewe mfano wale wasio na asili ya kiarabu huko Darfur au Watutsi nchini Rwanda. Ni dhahiri kwamba katika mifano yote hiyo wakosa wakubwa ni madikteta na tawala zizo za kisheria. Lakini kwa Wapalestina, wao ni mfano wa demokrasia pekee inayoweza kuzungumzwa katika eneo la mashariki ya kati, kama hali ilivyo kwa upande wa Israel.

Lakini wakati waisraili wanaishi likiwa ni taifa lenye ufundi wa halki ya juu na nguvu za kijeshi, umma ukiwa na kila aina ya uhuru , wapalestina bado wako katika hali ya umasikini mkubwa. Miaka iliopita imeshuhudia hali za kimaisha za wapalestina na haki zao zikizidi kupiga hatua ya kurudi nyuma. Wakati huo huo mwenendo wa amani umezidi kutoa matumaini madogo mno sawa na kukata tamaa juu ya uhuru na mustakbali wao.

Kukosa bahati kwa wapalestina lianza kitambo. Ni “ janga” lilioko tangu kuundwa dola ya Israel. Wapalestina wengi waliihama ardhi yao kuwa wakimbizi, wakipoteza sio tu ardhi bali pia mfumo wao wa kijamii na utamaduni wao. Kuweza kukidhi mahitaji yao, umma huo unalazimika kutegemea kazi ikiwa ni pamoja na katika sekta ya Ujenzi nchini Israel kujipatia fedha za kuishi.

Bila shaka kuundwa kwa dola ya Israel baada ya Uingereza kuacha mamlaka yake na umoja wa mataifa kupendekeza kugawanywa ardhi ya Palestina,kufuatia kuuawa kwa mamilioni ya Wayahudi na wanazi wa Ujerumani ya wakati ule. Hayo yaliwapa taifa Wayahudi na nafasi ya usalama kwa umma wake. Lakini Wapalestina walilazimika kuihama ardhi yao na kuilipia haki yao.

Ni kutokana na hali hiyo, leo ni siku ya umoja wa mataifa ya mshikamano na umma wa wapalestina. Hapana budi kunapaswa kufanywa kila juhudi ili nao waweze kuwa na taifa lao na nafasi ya kuishi. Kwa Ujerumani ina jukumu kubwa zaidi la kutoa mchango wake kuliko mataifa mengine katika umoja wa mataifa. Wajibu huo ni wa kihistoria. Ni wajibu ule ule ilionao mbele ya taifa la Israel, ndiyo unaopaswa kuupigania ili wapalestina nao wawe na taifa lao.