1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Simba wanne waingia mitaani Afrika Kusini

Sudi Mnette
11 Julai 2017

Nchini Afrika Kusini wakaazi katika baadhi ya vijiji vinavyozunguka mbuga ya wanyama wa Kruger wanaishi kwa mashaka baada ya simba wanne kutoroka katika mbuga hiyo na kuingia katioka maeneo ya makazi ya watu.

https://p.dw.com/p/2gMHb
Brüllende Löwen mit aufgerissenem Löwenmaul
Wanyama aina ya simba wakiwa katika hifadhiPicha: picture-alliance/dpa

Hali ilikuwa ya tafrani juma baada simba wanne kutoroka katika mbuga kubwa kabisa wanyama ya Kruger nchini Afrika. Madume manne ya simba yalitoroka Jumapili iliyopita kutoka katika mbuga hiyo, ambayo ni kivutio kikubwa kabisa cha utalii. Hali imekuwa ya kuchunguliwa milangoni kabla ya kutoka katika majumba yao kwa baadhi ya wakazi katika vijiji vilivyopo karibu na mbuga hiyo. Kataka taarifa yake ya awali mamlaka ya uhifadhi wa mbuga za wanyama nchini Afrika Kusini, simba hao walionekana katika kijiji cha Matsulu. Maeneo yanayozunguka mbuga ya Kruger yanajumuisha vijiji kadhaa na mashamba ya kukukuzuia mifugo, jambo ambalo kwa uhakika limewaweka watu wengi na mifugo yao katika hali ya wasiwasi wa kushambuliwa. Lakini hili si tukio la mara ya kwanza Mei, wahifadhi waliwatia mbaroni simba watano waliokuwa wametoroka. Mwaka 2015 simba maarufu katika mbuga nyingne tofauti na hiyo alipenya katika uzio wa umeme na kwa takribani wiki tatu akawa anauwa ngo'ombe kabla ya kukamatwa na askari wa wanyamapori.