1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Slovenia yachukua urais wa umoja wa Ulaya.

1 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CieG

Ijubijana. Slovenia imechukua wadhifa wa urais wa umoja Ulaya leo. Kosovo na kuidhinishwa kwa katiba mpya ya umoja huo huenda ikawa ajenda muhimu katika uongozi wa nchi hiyo. Taifa hilo dogo la Ulaya ya kati linachukua urais huo kutoka Ureno, na itaushikilia kwa muda wa miezi sita kabla ya kuipatia Ufaransa hapo Julai mosi. Slovenia inapanga kutumia historia yake kama jimbo la zamani la Yugoslavia ya zamani kuwa kama daraja baina ya umoja wa Ulaya na mataifa ya eneo la Balkan , wakati Kosovo inatishia kujitangazia uhuru kutoka Serbia . wakati huo huo Cyprus na Malta zimejiunga rasmi katika nchi zinazotumia sarafu ya Euro.