1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SOFIA.Duru ya pili ya uchaguzi kufanyika jumapili ijayo

23 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD05

Idadi ndogo ya wapiga kura waliojitokeza katika uchaguzi wa Bulgaria itamlazimu kiongozi wa nchi hiyo Georgy Parvanov kushiriki katika duru ya pili ya uchaguzi itakayo fanyika mwishoni mwa wiki ijayo, ijapo kuwa rais Parvanov alipata ushindi wa zaidi ya asilimia 60 katika duru ya kwanza.

Ni asilimia 40 pekee kati ya wapiga kura milioni 6.4 walioshiriki katika zoezi la kupiga kura hapo jana.

Kwa mujibu wa sheria za Bulgaria idadi hiyo ni chini ya kiwango kinachohitajika kuunda seikali.

Mpinzani wa rais Georgy Parvanov bwana Volen Siderov ni mpinzani wa umoja wa ulaya.

Hata hivyo yoyote atakae shinda katika duru ya pili ya uchaguzi wa jumapili ijayo ataiongoza Bulgaria inayotarajiwa kujiunga katika umoja wa ulaya januari mwaka ujao.