1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Soka Barani Afrika - Ni Zaidi ya Mchuano

2 Agosti 2010

Soka inavutia. Soka inaburudisha. Hata hivyo, katika maeneo ya watu maskini, wakati mwengine soka ndio kimbilio litakaloyabadili maisha.

https://p.dw.com/p/OaLy
Vijana wakicheza soka mtaaniPicha: LAIF

Kwa bahati mbaya, harakati hizo zinaweza kuingia doa pale watu walio na nia mbaya wanajaribu kuwatumia vibaya wanaojaribu kuitimiza ndoto hiyo.

Katika sehemu nyingi barani Afrika, ni jambo la kawaida kuwaona wanawake wametulia wakitazama runinga au kusikiliza redio kwa makini ili kufuatilia mechi na michuano inayoendelea. Ni kawaida kuwaona wachezaji chipukizi katika viwanja vingi vya michezo barani Afrika, wakiwa wamevalia jezi za wachezaji maarufu wa timu za kimataifa kwa mfano Barcelona ya Uhispania au Manchester United ya Uingereza. Kwa mara ya kwanza kabisa, kinyang'anyiro cha kuwania kombe la dunia kilifanyika mwezi wa Julai mwaka 2010 barani Afrika nchini Afrika Kusini. Bara zima lilisisimka kwa furaha!

Wachezaji maarufu wa soka walio na asili ya Afrika huwatia wengi barani humo moyo na kuwafanya kujiuluza: Ikiwa Drogba, Eto'o na Essien wamefanikiwa kucheza soka ya kulipwa, kwa nini na mimi nisifanikiwe?

Chedede, Jonathan na Safina, washiriki wakuu katika mala hii ya redio,wanatokea kwenye jamii tofauti ila wana ndoto moja wanayotaka kuitimiza: kupata nafasi kuwa mcheza kandanda stadi kote ulimwenguni.

Ungana nao katika safari hii yao ngumu ili ujue ikiwa watafanikiwa.Wengi huteuliwa ila ni wachache wanaochaguliwa.Ifahamike kuwa kila mchezo unakabiliwa na changamoto za kila aina za rushwa na ufisadi,mivutano ya uongozi na hata ulafi.

Michezo ya Noa Bongo: Jenga Maisha yako inaweza kusikilizwa katika lugha sita tofauti: Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kihabeshi. Mradi huu unaungwa mkono na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani.