1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Solana akatishwa tamaa na Iran

1 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVPO

LONDON.Mkuu wa siasa za nje wa Umoja wa Ulaya, Javier Solana amesema kuwa amevunjika moyo baada ya mazungumzo yake na msuluhishi wa Iran juu ya mzozo wa nuklia wa nchi hiyoSaeed Jalili.

Mazungumzo hayo yaliyofanyika jijini London, yamefanyika kabla ya Umoja wa Ulaya haujawasilisha ripoti yake Umoja wa Mataifa juu ya mpango wa nuklia wa Iran.

Mazungumzo hayo pia yalionekana kama nafasi ya mwisho kwa kubatilisha mbinyo wa Marekani kutaka vikwazo vikali zaidi vya kimataifa dhidi ya Iran.

Umoja wa Mataifa unaitaka Iran kusitisha mpango wake huo wa uzalishaji wa madini ya uranium.

Iran inasisitiza kuwa mpango wake huo ni kwa ajili ya shughuli za kawaida, lakini nchi za magharibi zikiongozwa na Marekani zinawasi wasi kuwa nchi hiyo huenda ikatengeza silaha.