1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia baada ya kuchaguliwa Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais

12 Septemba 2012

Mapema wiki hii, wabunge wa Somalia walimchagua Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais mpya wa nchi hiyo katika mchakato unaoelezwa kuwa hatua kubwa kwa nchi iliyokabiliwa na miongo miwili ya vita, machafuko na ukimbizi.

https://p.dw.com/p/167Cx
Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Muhamud (katikati)
Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Muhamud (katikati)Picha: picture-alliance/dpa

Kwa kuzingatia changamoto nyingi zinazobakia nchini Somalia, je Rais Mohamud anatoa matumaini kwa mamilioni ya wakimbizi wa Kisomali hatimaye kuweza kurejea nyumbani? Daniel Gakuba anazungumza na Hussein Bantu, mbunge aliyeko mjini Mogadishu, ambaye pamoja na mengine anaelezea hali ya jumla ilivyo sasa nchini Somalia baada ya kuchaguliwa kwa Rais Mohamud.

(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: Daniel Gakuba
Mhariri: Mohammed Khelef