1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia: Baada ya miongo miwili ndege ya kimataifa yatua Mogadishu

6 Machi 2012

Nchini Somalia,Baada ya miongo miwili hatimae leo (06.03.2012) ndege ya kwanza ya Kibiashara ya Kimataifa ya shirika la ndege la Uturuki imewasili katika uwanja wa ndege wa mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.

https://p.dw.com/p/14Fi0
Ndege la shirika la Uturuki yatua uwanja wa ndege wa Mogdishu
Ndege la shirika la Uturuki yatua uwanja wa ndege wa MogdishuPicha: AP

Naibu waziri mkuu wa Uturuki aliyekuwa mmoja wa abiria katika ndege hiyo Bekir Bosdag amesema nchi yake imeanzisha rasmi shughuli za shirika hilo la ndege nchini Somalia.Hali ya usalama iliimarishwa katika uwanja huo wa ndege mapema leo asubuhi kabla ya kutua ndege hiyo iliyotokea Ankara.

Saumu Mwasimba amezungumza moja kwa moja kutoka Mogadishu na mbunge Hussein Bantu ambaye pia alikuweko kuwalaki wageni kutoka Uturuki na kwanza amezungumzia hisia zake juu ya kuwasili kwa ndege hiyo.

(Kusikiliza mazungumzo hayo, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi : Saumu Mwasimba

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman