1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia kuwekeza katika bandari yake ya Kismayu

Admin.WagnerD4 Desemba 2013

Licha ya serikali ya Somalia kafanya jitihada za kuikarabati bandari ya Kismayu, mpaka sasa bado bandari hiyo inatumiwa kama njia kuu ya kupitishia dawa za kulevya kutoka Asia na uendeshaji wa biashara nyingi haramu.

https://p.dw.com/p/1ATA6
Meli iliyotekwa katika eneo la Bahari nchini Somalia
Meli iliyotekwa katika eneo la Bahari nchini SomaliaPicha: picture-alliance/dpa

Bandari ya Kismayu iliyopo karibu kabisa na kaskazini mwa Kenya na Ethiopia, ni moja wapo ya bandari yenye kina kirefu kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki, ambayo ina uwezo wa kubeba tani nyingi za mizigo, kwa miongo kadhaa sasa imekuwa ikitumika kama njia kuu ya biashara haramu zinazoingia na kutoka katika ukanda mzima wa nchi za Afrika Mashariki.

Udhibiti pekee utaiwezesha Somalia kuingiza pato zuri katika Bandari zake

Ingawa dola ya kimataifa imejikita katika kudhiti biashara ya mkaa inayofanywa na kundi la al-shabaab katika bandari ya Kismayu, ambayo ndio biashara pekee inayotegemewa na kundi hilo kwa kipato, lakini bado inafanyika. Afisa mmoja wa kibalozi ambaye hakutaka jina lake litangazwe, amesema watu kadhaa wamekuwa wakijipatia kiasi kikubwa cha fedha kupitia bandari hiyo, ambapo ingekuwa inasimamiwa ipasavyo bila rushwa ya viongozi, ingaliweza kuingiza kiasi kikubwa cha mapato ya ushru kwa serikali

Ukarabati wa bandari hiyo hautakuwa na manufaa ya kuongeza pato la ushuru pekee kwa serikali na kundi la Madobe lililosaidia serikali ya Somalia kuwang'oa al-Shabaab, bali pia udhibiti utakaokuwepo utaweza kukatiza shughuli zote haramu zinazoendeshwa na kundi hilo katika bandari hiyo.

Msemaji wa rais wa Somalia, Abdirahman Omar Osman,amewaambia shirika la habari la Reuters kuwa, rais wao anataka kusiwepo kabisa na vitendo vya rushwa na utawala bora lakini bado watu wake walio waaminifu ni wachache, jambo ambalo limemfanya rais kuomba msaada wa kupambana na rushwa nchini mwake kutoka jumuiya ya kimataifa.

Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud
Rais wa Somalia, Hassan Sheikh MohamudPicha: Getty Images

Magunia milioni moja ya mkaa kuvushhwa kinyemera kila mwezi

Wapelelezi wa umoja wa mataifa katika eneo hilo, wamesema tangu mwezi July, kumekuwa na takribani magunia milioni moja ya mkaa yakipitishwa kila mwezi kutoka bandari hiyo, yenye thamani ya dala milioni 15 hadi 16. Na hayo yote yamekuwa yakitendeka baada ya kundi la Ras Kamboni na askari kutoka Kenya kuikomboa Somalia kutoka utawala wa Al-shabaab

Hata hivyo kuna taarifa kuwa katika bandari hiyo kuna makundi matatu yanayoendesha biashara kinyemera ambayo ni baadhi ya wanajeshi wa kenya, wanamgambo wa kundi la Ras kamboni linaloongozwa na Madobe na wanamgambo wa kundi la al-shabaab,licha ya kwamba walikuwa katika mapigano.

Afisa mwingine wa kibalozi, anayefanya karibu na eneo hilo, ambaye naye hakuta kutaja jina lake,amesema ingawaje kumekuwa na kile kinachodaiwa udhibiti uliofanywa na askari wa madobe na kenya,lakini kimsingi hakuna mabadiliko ya shughuli haramu katika bandari hiyo, ingawaje afisa mwingine wa kibalozi anasema kuwa, maafisa wa jeshi la kenya ndio suluhisho pekee la udhibiti wa eneo hilo.

Haramia wa kisomali kwenye fukwe za eneo Kismayu
Haramia wa kisomali kwenye fukwe za eneo KismayuPicha: picture-alliance/AP

Taarifa za kiusalama zinasema kuwa, njia za panya za biashara haramu kutoka bandari ya kismayu mpaka eneo la Garisa nchini Kenya, zimekuwa zikipitisha sukari, vifaa vya umeme, dawa za kulevya na silaha kutoka Afghanistan na Pakistan.

Mpaka sasa nchi kadhaa zimeonyesha nia ya kuwekeza katika mradi wa bandari hiyo ya Kismayu, ambapo ukarabati wake utahitaji kiasi cha takribani dala za kimarekani 250 na nchi itakayoingia ubia itakuwa na haki miliki ya kati ya miaka 25 hadi 50. Nchi zilizojitokeza kwa nia ya kuwekeza katika mradi huo ni China, Uturuki, Kenya, Afrika kusini na Marekani

Mwandishi: Diana Kago/REUTERS
Mhariri: Abdul-Rahman