1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia: Uchaguzi wa Rais waahirishwa

20 Agosti 2012

Zoezi la kumchagua rais wa Somalia ambalo lilitarajiwa kufanyika leo hii (20.08.2012) limeshindikana kutokana kuwepo kwa mzozo katika zoezi la kuchagua wabunge 275 taifa hilo.

https://p.dw.com/p/15ssT
Mgombea wa urais Somalia, Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed Ali
Mgombea wa urais Somalia, Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed AliPicha: Reuters

Miongoni mwa wagombea wanaopewa nafasi kubwa kushinda, ni rais wa sasa wa serikali ya mpito, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed Ali na Spika anayemaliza muda wake, Sharif Hassan Sheikh Adan. Sudi Mnette alizungumza moja kwa moja kutoka Somalia na mwenzetu Hussein Awes na kwanza alimuuliza Rais wa Somalia atapatikana kama ilivyopangwa?

(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: Sudi Mnette

Mhariri: Othman Miraji