1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia yagonga vichwa vya habari

28 Desemba 2006

Wahariri wa magazeti ya leo ya Ujerumani waliichambua kwa mapana na marefu Somalia pamoja na azma ya Ethiopia na masilahi yake kujitumbukiza Somalia.

https://p.dw.com/p/CHU7

Gazeti la ALLGEMEINE ZEITUNG kutoka Mainz laandika:

„Kile kinachopita sasa katika Pembe ya Afrika, si kingine bali jaribio la waislamu wakakamavu kutoka nchi mbali mbali –baada ya Afghanistan,Irak na Palestina-kufungua safu mpya ya vita kwa shabaha ya kuunda dola la kiislamu.Ethiopia inapigana katika kitovu cha Afrika sio dhidi ya umma wa wasomali,bali dhidi ya wachechnia,wapakistani na waarabu wa uraia tofauti .

Hii inadhihirisha zaidi kuliko kitu kingine zaidi ,nani yuko nyuma ya balaa hili-ni mtandao wa Al kaida.“Ni maoni ya Allgemeine Zeitung kutoka Mainz.

Gazeti la Financial Times la Ujerumani, linhisi kuwa, wanamgambo wa kiislamu huko Somalia baada ya umwagaji damu wa siku chache zilizopita kwa sasa hawtakua tayari kwa mazungumzo ya amani .Amani na utulivu lakini,ndio masharti ya kimsingi kuizuwia Somalia isitumbukie zaidi katika mtandao wa waislamu wenye itikadi kali ulimwenguni.

Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linalochapishwa mjini Munich linashauri Umoja wa Afrika na Jumuiya ya nchi za kiarabu-Arab League –zibebe jukumu la upatanishi.Laandika:

„Wanamgambo wa kiislamu kujumuishwa ndani ya serikali mpya ya Somalia kunatoa fursa ya kuviimarisha vikosi vya wastani.Kwani, ni muafaka tu utakaogawa madaraka pande zote mbili,ndio utakaofungua njia ya kuzima itikadi kali .“

Ama gazeti la VOLKSSTIMME mjini Magdeburg linatufunulia kawa Ethiopia ina masilahi gani katika kujiingiza katika mzozo wa somalia:Laandika:

„Ethiopia nchi ya kikristu kwanza kabisa azma yake ni kuiona Somalia haiangukii mikononi mwa waislamu wenye itikadi kali ya kiislamu.

Kwani dola hili kubwa lenye nguvu katika Pembe ya Afrika kwa kupotelewa na Eritrea,imedhofika na kuwa nchi isiopakana na bahari.Kujipatia sasa upenu wa kuwasili pwani kupitia Somalia kunaiweka Ethiopia katika hali nzuri kabisa kimkakati.“-lasema gazeti hilo la mjini Magdeburg.

Mwishoe, gazeti la TAGESSPIEGEL linalochapishwa mjini Berlin,linamurika msimamo wa serikali ya Ujerumani juu ya mzozo huu katika Pembe ya Afrika:

Laandika:

„Ujerumani ambayo inapiga doria na manuwari zake katika pwani ya Somalia kupitia ule mpango wa kupiga vita ugaidi-Enduring Freedom-hadi sasa imejiweka kando ya mgogoro huu.

Nyuma ya pazia lakini, Ujerumani inaiungamkono serikali ya Somalia inayotambuliwa kimataifa kibaraka wa Ethiopia .

Kuelemea huko upande mmoja sasa kukome.Waziri wa ulinzi Bw.Jung hamudu tena kuiingiza Ujerumani na vikosi vyake katika vita vyengine vya kienyeji na hasa ikizingatia jukumu lake la kuja kuwa mpatanishi. Januari,mwakani,Ujerumani, sio tu itakuwa mwenyekiti wa kundi la dola kuu 8 za kiviwanda-G-8 bali pia wa Umoja wa Ulaya.