1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SPLA yadai kushambuliwa na vikosi vinavyoungwa mkono na serikali ya Khartoum

24 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cfri

JUBA:

Wanamgambo wakisaidiwa na jeshi la Khartoum inasemekana wamewashambulia wanajeshi wa jeshi la Sudan Kusini na kuwauwa watu kadhaa.

Kwa mujibu wa maofisa wa jeshi la Sudan Kusini, shambulio hilo limetokea karibu na mpaka wa eneo la kaskazini na la kusini mwa Sudan.

Meja Generali James Hoth,wa kundi la zamani la wapiganaji wa kusini mwa nchi hiyo la SPLA ,amesema kuwa ushirika wa wapiaganaji wa Murahaleen na Popular Defence Forces-PDF ukisaidiwa na baadhi ya wanajeshi wa jeshi la serikali la SAF, ndio wameafanya shambulio hilo.Anaongeza kuwa kambi ya SPLA ilishambuliwa lakini wavamizi walirejeshwa nyuma.

Aidha anasema anafikiri shambulio hilo limesababishwa na hali ya wasiwasi ilioko katika eneo hilo akisema , huenda kuna waliowaambia kuwa SPLA imevuka mpaka ambao ilikuwa inapashwa kuwa .Hata hivyo jeshi la serikali pamoja na lile la PDF limekanusha kuhusika na shambulio hilo. Idadi ya waliofariki haijajulikana lakini msemaji wa SPLA -Kuol Diem -Kuol amesema ameambiwa na asakari wake kuwa watu 70 ndio wameuawa .