1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SREBRENICA: Mabaki ya Waislamu kuzikwa leo

11 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjy

Mabaki ya waislamu zaidi ya 450 waliouwawa miaka 12 iliyopita huko Srebrenica, katika mauaji mabaya zaidi kuwahi kufanywa barani Ulaya tangu kumalizika kwa vita vya pili va dunia, yatazikwa hii leo.

Manusura kiasi ya 30,000 na jamaa za wahanga wanatarajiwa kuhudhuria maziko hayo kwenye eneo la makaburi ambako maiti nyingine za watu zaidi 2,400 waliouwawa wakati huo, zilizikwa.

Muongozaji mkuu wa mashtaka ya uhalifu wa kivita wa Umoja wa Mataifa, Carla Del Ponte, atahudhuria maziko hayo.

Mabaki ya watu 465 yaliyopatikana kwenye makaburi ya halaiki huko Srebrenica, yametambuliwa kupitia kipimo cha nasaba, DNA.

Mwishoni mwa vita vya Bosnia kati ya mwaka wa 1992 na 1995, vikosi vya Serbia viliivamia Srebrenica na kuwaua Waislamu takriban 8,000 wanaume na vijana.