1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sri Lanka yasitisha makubaliano ya amani na waasi wa Tamil

3 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cjso

COLOMBO

Wasimamizi wa amani wa nchi za Scandinavia leo wamekuwa wakijiandaa kuondoka Sri Lanka wakati serikali ya nchi hiyo ikisema kwamba itaijulisha rasmi Norway juu ya uamuzi wake wa kujitowa kwenye makubaliano ya amani kati yake na waasi wa Tamil Tiger yaliodhaminiwa na Norway.

Waziri wa habari Anura Yapa amewaambia waandishi wa habari leo hii kwamba serikali imeamuwa kuachana na makubaliano hayo kwa sababu hayafanyi kazi na hayatakelezeki kama njia ya kukomesha mzozo wa kikabila uliodumu kwa miongo miwili nchini humo.

Masaa mchache kufuatia tangazo la serikali kujitowa kwenye makubaliano hayo ya amani kumezuka mapigano makali kaskazini mwa Sri Lanka ambapo waasi saba wa Tamil Tiger na mwanajeshi mmoja wa serikali wameuwawa.