1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier asisitiza majadiliano Ukraine

Admin.WagnerD13 Mei 2014

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amesema uchaguzi wa rais nchini Ukraine Mei 25 utakuwa muhimu katika kuiondoa nchi hiyo kwenye mgogoro, na kuutaka utawala mjini Kiev kukaa na waasi.

https://p.dw.com/p/1Bymb
Steinmeier in Kiew mit Jazenjuk 13.05.2014
Picha: Reuters

Waziri Steinmeier ameyasema hayo baada ya kuwasili mjini Kiev kuunga mkono majadiliano ya kitaifa, yenye lengo la kukomesha mgogoro wa nchi hiyo. Steinmeier alisema huenda akasafiri pia hadi mashariki mwa Ukraine kujaribu kujenga daraja kati serikali mjini Kiev na waasi wanaotaka kujitenga.

Waziri Steinmeier alipokelewa na waziri mkuu Arseniy Yatsenyuk kwenye uwanja wa ndege wa Kiev kabla ya kuendelea na safari kuelekea mji wa Odessa uliyoko katika bahari Nyeusi, ambako mapigano makali yalitokea kati ya vikosi vya Ukraine na waasi.

Majimbo ya Donestk na Luhansk yalipiga kura Jumapili kuhusu uhuru kutoka kwa Ukraine.
Majimbo ya Donestk na Luhansk yalipiga kura Jumapili kuhusu uhuru kutoka kwa Ukraine.Picha: Reuters

Asisitiza umuhimu wa majadiliano

Swaziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani amesema hali katika baadhi ya maeneo ya Ukraine bado ni hatari na ya kutisha, na kusisitiza umuhimu wa majadiliano kati ya viongozi mjini Kiev, na waasi wanaotaka kujitenga mashariki mwa nchi hiyo, ambako majimbo mawili yalipiga kura ya uhuru kutoka Kiev mwishoni mwa wiki. Kura hiyo ya maoni ambayo haichukuliwi kuwa batili na utawala mjini Kiev tu - lakini pia na Umoja wa Ulaya na Marekani, inatishia kuivuruga zaidi nchi hiyo ya Ulaya mashariki.

Waziri Steinmeier aliwatolea wito maafisa kuhakikisha kuwa raia wengi kadiri iwezekanavyo wanajitokea kushiriki katika uchaguzi ujao wa Mei 25, ambao alisema unaweza kusaidia kupunguza wasiwasi. Kiev imekuwa ikiongozwa na serikali ya muda tangu kuondolewa kwa rais Viktor Yanukovych mwezi Februari kufuatia maandamano yaliyodumu miezi kadhaa.

Ziara ya Steinmeier imekuja siku chache tu baada ya wanaharakati wanaotaka kujitenga katika majimbo ya mashariki ya Donetsk na Luhansk kuendesha kura ya maoni ili kuwa majimbo huru. Siku ya Jumatatu, kiongozi wa wanaoiunga mkono Urusi katika mji wa Donetsk Denis Pushilin, alisema kura hiyo aliakisi matakwa ya raia, na kuiomba Urusi iliingize jimbo hilo katika shirikisho lake.

Kiongozi wa 'Jamhuri yawatu wa Donetsk' Denis Pushilini ameiomba Urusi kulifanya jimbo hilo kuwa sehemu ya shirikisho lake.
Kiongozi wa 'Jamhuri yawatu wa Donetsk' Denis Pushilini ameiomba Urusi kulifanya jimbo hilo kuwa sehemu ya shirikisho lake.Picha: Reuters

Waziri mkuu wa muda Yetsenyuk pia aliuzungumzia mgogoro wa nchi yake kufuatia mkutano wa Steinmeier. Alisisitiza hata hivyo kwamba Urusi laazima isitishe msaada wa kisiasa kwa makundi ya wanaotaka kujitenga, na kuongeza kuwa ni Moscow na waka siyo Kiev inayoshikilia ufunguo wa kuituliza tena Ukraine.

Kiev haitaki kujadiliana na "magaidi"

Matukio yanayojulikana ya ushiriki wa Urusi tayari yamezilaamisha Marekani na Umoja wa Ulaya kuwawekea vikwazo vya usafiri na kuzuwia mali za washirika wa karibu wa rais Vladmir Putin. Awamu ya hivi karibuni ya vikwazo hivyo ilitangazwa baada ya kura ya Jumapili, kutokana na kutokuwepo hatua zozote za kupunguza mgogoro mashariki mwa Ukraine na Urusi.

Waziri mkuu Yatsenyuk pia alikaribisha ushiriki wa mwanadiplomasia wazamani wa Ujerumani Wolfgang Ischinger katika majadiliano yanayoanza kesho Jumatano, lakini alitofautiana na mtazamo wa Steinmeier wa namna ya kuyasukuma mbele mazungumzo hayo, akipendelea ruwaza ya awali ya ushiriki wa Ukraine, Urusi, Umoja wa Ulaya na Marekani na kuwaweka kando 'magaidi' wanaotaka kujitenga.

Mwandishi: Iddi Ssessanga/rtre,afpe, ape, DW
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman