1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier na Solana kukutana na Condoleezza Rice mjini Washington

Josephat Charo19 Machi 2007

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, na mratibu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Javier Solana, wamo mjini Washington, Marekani kwa ziara fupi.

https://p.dw.com/p/CHHw
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani Frank Walter SteinmeierPicha: AP

Frank Walter Steinmeier na Javier Solana wanatarajiwa kukutana hii leo na waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice mjini Washington Marekani kujadili njia za kuziendeleza juhudi za kutafuta amani ya Mashariki ya Kati. Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na uhusino na mataifa ya kigeni, Benit Ferrero Waldner, atashiriki katika mazungumzo hayo.

Ushirikiano baina ya Umoja wa Ulaya na Marekani unatarajiwa kuwa mada kuu katika mazungumzo ya mjini Washington. Je mazungumzo hayo yataondoa wasiwasi uliopo Ulaya juu ya mpango wa Marekani kuwepa makombora yake nchini Poalnda na Chechnya? Karsten Voigt, mratibu wa ushirikiano baina ya Marekani na Ujerumani alitoa matamshi haya.

´Kinachonivutia ni kwamba kwa wakati huu nchini Urusi, Poland Chechnya, Ujerumani na hata Marekani, ushirikiano unatafutwa tena kutoka wakati wa mikataba ya shirika la NATO na mfumo wa ulinzi wa maroketi wa rais wa zamani wa Marekani, Ronald Reagan. Hilo linaeleweka ila njia za kuyafanya mazungmuzo haya ni tofauti kabisa ukilinganisha na wakati wa vita baridi. Na ndio maana kunahitajika uangalifu mkubwa na sio tu kusema tunahitaji kuwa na muungano kama zamani. Kusema kweli kunaweza kuleta matokeo mabaya.´

Akiondoka mjini Berlin waziri Frank Walter Steinmeier ametakiwa kulijadili kwa kina swala la mfumo wa ulinzi wa maroketi ya Marekani barani Ulaya. Mpango huo umezusha hali ya kutoelewana katika serikali ya Ujerumani.

Kansela wa Ujerumani, Bi Angela Merkel, ameonya juu ya mpango huo wa Marekani akisema uamuzi wa taifa binafsi la Umoja wa Ulaya hautaleta manufaa. Bi Merkel ametaka kuwepo mkutano baina ya Umoja wa Ulaya na Marekani ili kuepusha malumbano kuhusiana na mpango huo.

Mkutano huo unafanyika wakati ambapo Marekani inaibinya serikali mpya ya Wapalestina itimize masharti ya kimataifa, ikisema itaitambua iwapo itakubali kuachana na machafuko na kuitambua kikamilifu Israel.

Mshauri wa maswala ya usalama wa kitaifa nchini Marekani, Stephen Hadley, alitangaza msimamo huo mkali hapo jana baada ya waziri mkuu wa mamlakaa ya Palestina, Ismail Haniyeh, kusisitiza juu ya haki ya serikali yake ya aina zote za upinzani hivyo kukataa sharti muhimu litakaloiwezesha serikali hiyo itambulike.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema amevunjwa moyo na ripoti zilizotolewa na serikali mpya ya mamlaka ya Palestina. Pande nne zinazohusika na mpango wa amani ya Mashariki ya Kati zikiwemo Marekani, Urusi, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya, zimerudia msimamo wao kwamba serikali mpya ya mamlaka ya Palestina sharti ikubali mikataba iliyosainiwa hapo awali na iyalaani machafuko.

Ziara ya Frank Walter Steinmeier na Javier Solana mjini Washington inatarajiwa kuleta mwelekeo mpya Mashariki ya Kati.