1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier Ziarani Goma

20 Februari 2015

Ujerumani imeahidi kukuza uhusiano wake na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Ahadi hiyo imetolewa mjini Kinshasa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier.

https://p.dw.com/p/1Ef01
Waziri wa nje wa Ujerumani Frank Walter- Steinmeier na Rais Joseph Kabila Kabange
Waziri wa nje wa Ujerumani Frank Walter- Steinmeier na Rais Joseph Kabila KabangePicha: picture-alliance/dpa/M. Kappeler

► Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier,yuko ziarani nchini Kongo ambako amesema uhusiano kati ya nchi yake Ujerumani na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ni hasa wa kiuchumi na kimazingira. Euro milioni 235 zimeahidiwa kutolewa kwa ajili ya kuboresha sekta ya kilimo nchini Kongo, lakini msaada huo utatolewa mara tu bunge la Kongo litakaporekebisha kanuni za uwekezaji kwenye sekta ya kilimo.

Licha ya migogoro inayoikumba ulimwengu,tunatakiwa kujihusisha na kinachoendelea barani afrika kwa ujumla na nchini DRC kwa upekee,alisema kwenye mkutano na wandishi habari hapa mjini Kinshasa ,Frank-Walter Steinmeier. Waziri wa mambo ya nje wa ujerumani ambae anaongozana na ujumbe wa watu 120 wakiwemo wabunge na wafanya biashara, amesema ziara yake nchini Kongo inahusu maswala ya uhusiano na kiuchumi:Tunanukuu

« Kuhusu uhusiano wa nchi zetu mbili,tulielezea kwamba kunamahitaji ya kila moja wetu.Kuna umuhimu mkubwa wa kufikia maendeleo kupitia kubadilishana ujuzi na maarifa baina ya nchi mbili hizi,lakini bado kunachangamoto kubwa ikiwa Kinshasa au Berlin ».

Kwa upande mwingine ,ujerumani imepongeza kutangazwa kwa kalenda ya uchaguzi.Lakini waziri Steinmeier amesema msaada kwa ajili ya uchaguzi utatokana na mahitaji ya serikali ya Kongo kupitia taasisi za umoja wa ulaya ambayo Ujerumani ni nchi mwanachama. Waziri wa Kongo wa mambo ya nje,Raymond Tsibanda alisema msaada wa ujerumani hivi sasa nchini Kongo unatolewa kwenye sekta ya mageuzi ya jeshi na polisi,na rasilimali na sekta ya kibinafsi:

«Tupo tayari kwa ushirikiano na ujerumani kwenye sekta nyingi za uwekezaji,na tumehimiza wafanya biasahara wa kijerumani kujitokeza kwa wingi.Tunataka ushirikiano wa kila upande kufaidika».

Frank Walter- Steinmeier alikuwa na mashauriano na rais Joseph Kabila na waziri mkuu Matata Ponyo.Wafanya biashara wa Ujerumani walikutana na maafisa wa serikali pamoja na wafanya biashara wenzao wa Kongo.Halter Dieter Walter,kiongozi wa ujumbe wa wafanya biashara wa Ujeruamani alisema kwamba nchi yake itataoa msaada wa Euro milioni 235 ilikuboresha sekta ya kilimo nchini Kongo.

Wachimba migodi mjini Goma
Wachimba migodi mjini GomaPicha: picture-alliance/dpa

Lakini fedha hizo zitatolewa endapo bunge la Kongo litarekebisha kanuni za uwekezaji kwenye sekta ya kilimo.Hapo jana waziri Steinmeir alizindua kituo kipya cha mafunzo ya kijerumani ,Goethe Institute.

Waziri Frank Walter-Steinmeier atahitimisha ziara yake nchini Kongo baadae leo(20.02.2015) mjini Goma,jimboni Kivu ya kasakazini.Steinmeier anatazamiwa kuanzisha kazi za ukarabati wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Goma ambao umefadhiliwa na serikali ya Ujerumani.

Baadae atazuru kambi ya wakimbizi ya Mugunga III,kituo cha afya cha Kibati na hospitali ya shirika la kijerumani la Johanniter Unfallhilfe.

Mwandishi:Saleh Mwanamilongo,DW Kinshasa.

Mhariri:Yusuf Saumu