1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Stella Nyanzi arudishwa gerezani Uganda

Mohamed Dahman
27 Aprili 2017

Mahakama kuu nchini Uganda imemrejesha gerezani msomi na mkosoaji mkubwa wa Rais Yoweri Museveni bibi Stella Nyanzi.

https://p.dw.com/p/2c0Lc
Uganda Dr. Stella Nyanzi
Picha: Getty Images/AFP/G. Grilhot

Mahakama Kuu nchini Uganda imemrudisha gerezani msomi na mkosoaji wa Rais Yoweri Museveni na kufunguwa njia ya kufanyiwa uchunguzi wa akili wa lazima.

Stella Nyanzi mhadhiri na mtafiti wa chuo kikuu ametiwa gerezani zaidi ya wiki mbili zilizopita wakati nchi hiyo ya Afrika Mashariki ilipomfungulia mashtaka kuhusiana na makosa ya mtandaoni.Makosa hayo yanatokana taarifa alizoweka kwenye mtandao wake mashuhuri wa facebook ambapo amewashutumu Museveni na mke wake kwa kuvunja ahadi ya uchaguzi ya kutowa vitaulo vya wanawake vya kujistiri wakati wa kupata siku zao.

Mke wa Museveni ni waziri wa elimu nchini Uganda. Msomi  huyo alikuwa amefikishwa mahakama kuu kuomba dhamana baada mahakama moja ya chini kukataa kusikiliza kesi hiyo. Pia alikuwa akitaka mahakama hiyo kuu kuacha kuzingatia ombi la serikali la kutaka afanyiwe uchunguzi wa akili.