1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

STRASSBOURG: Mauaji ya ripota wa Kirussi yamelaaniwa

8 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4m

Baraza kuu la Umoja wa Ulaya limelaani mauaji ya mwandishi wa habari maarufu wa Kirussi,Anna Politkovskaya.Taarifa iliyotolewa na baraza hilo inasema,uuaji wa ripota huyo ni ishara ya kuwepo tatizo kuhusu uhuru wa usemi nchini Urussi. Politkovskaya amekuwa maarufu kwa ripoti zake za uchunguzi kuhusu hali halisi ya Chechnya na vitendo vya wanajeshi wa Kirussi katika jimbo la Chechnya linalogombea kujitenga na Moscow.