1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Stratford-upon-Avon, Uingereza. Mawaziri wapanga kupambana na imani kali na ugaidi.

27 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyv

Mawaziri wa mambo ya ndani kutoka nchi sita zenye idadi kubwa ya wakaazi barani Ulaya wamekubaliana katika mpango wenye hatua za kupambana na mashambulizi yanayopangwa ya kigaidi na kufanya msako dhidi ya uhalifu wa kupangilia.

Mawaziri hao kutoka Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Hispania , Italia na Poland , ambao wamekutana kwa muda wa siku ya pili katika mji wa Stratford-upon-Avon nchini Uingereza, wamesema kuwa wataongeza ushirikiano wao na kuchunguza mawasiliano ya Internet zaidi ili kujaribu kupambana na watu wenye imani kali pamoja na uhamiaji kinyume na sheria.

Nchi hizo pia zinania ya kushirikiana taarifa za kijasusi juu ya mabomu ya majimaji.

Taarifa kutoka katika mkutano huo imesema kuwa juhudi mahsusi zitalenga katika kuwapa nafasi vijana wa Kiislamu kuweza kufanikiwa katika jamii ya mataifa ya magharibi.

Sehemu ya ajenda ya mawaziri hao inahusu njia za kupambana dhidi ya kupata imani kali kwa vijana wa Kiislamu katika mataifa ya Ulaya na kuwaunga mkono zaidi wale wenye msimamo wa kati katika jamii ya Kiislamu.