1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan ya Kusini kutangazwa taifa huru

31 Januari 2011

Sudan ya Kusini, itatangazwa taifa huru na itajitenga na kaskazini, tarehe 9 mwezi wa Julai.

https://p.dw.com/p/QwqW
(FILE) A file picture dated 19 January 2010 shows Sudanese President Omar el Bashir (R) and First Vice President and President of the Government of Southern Sudan, Salva Kiir Mayardit (L), participating in celebrations marking the 5th anniversary of the signing of the Comprehensive Peace Agreement (CPA) in Yambio, Sudan. Omar el Bashir has won the country's first multiparty elections in 24 years, election officials said on 26 April 2010. The polls are supposed to usher in a new era of democracy in Sudan, which is recovering from a decades-long civil war between the north and south. EPA/TIM MCKULKA - UNMIS - HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES +++(c) dpa - Bildfunk+++ Verwendung nur in Deutschland, usage Germany
Rais wa Sudan ya Kusini, Salva KiirPicha: AP

Rais Salva Kiir wa eneo hilo la kusini lenye utawala wa ndani akitangaza habari hiyo, aliongezea kuwa Juba huenda ukawa mji mkuu wa taifa hilo jipya, litakalokuwa taifa la 54 barani Afrika na 193 duniani.

Kwa mujibu wa halmashauri ya uchaguzi, takriban asilimia 99 ya wapiga kura wa Sudan ya Kusini, walioshiriki katika zoezi la kura ya maoni, mwanzoni mwa mwezi huu, wameamua kujitenga na kaskazini. Maelfu ya watu walisherehekea matokeo hayo mjini Juba.

Mapema mwezi huu, Rais wa Sudan Omar al-Bashir alisema kuwa atatambua matokeo ya kura hiyo ya maoni ambayo ni sehemu ya makubaliano ya amani ya mwaka 2005. Makubaliano hayo yalimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka 22 nchini humo na kusababisha vifo vya zaidi ya watu milioni mbili na mamilioni wengine kupoteza makaazi yao.