1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan yakiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa kwa kupeleka silaha katika jimbo la Darfur

19 Aprili 2007

Umoja wa Mataifa umethibitisha habari kwamba serikali ya Sudan iliziwekea nembo ya Umoja wa Mataifa ndege zake ili kuweza kupeleka silaha katika jimbo la Darfur.

https://p.dw.com/p/CHFv
Darfur
DarfurPicha: AP

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa bwana Ban Ki- Moon amethibitisha habari kwamba serikali ya Sudan ilizitia rangi ya Umoja wa Mataifa ndege zake na hivyo kuweza kupeleka silaha katika jimbo la Darfur magharibi mwa nchi hiyo. Katibu Mkuun Ban Ki-Monn amelaani vikali kitendo hicho.

Msemaji wa katibu mkuu ameeleza kuwa matendo kama hayo ya Sudan ya kuzipaka ndege zake rangi na kuzitia nembo ya Umoja wa Mataifa ni kukiuka sheria za kimataifa na hadhi ya Umoja wa Mataifa.

Ndege hizo za jeshi la Sudan zilipeka silaha katika jimbo la Darfur. Madai hayo yamethibitishwa kwa picha. Ndege hizo za kirusi zilitiwa rangi nyeupe na kuwekewa herufi za Umoja wa Mataifa UN.

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa ndege hizo hazikutumika kwa ajili ya usafirishaji tu bali pia kwa ajili ya kufanyia upelelezi na mashambulio.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa katibu mkuu bwana Ban Ki-Moon anatumai kuungwa mkono ili mkasa huo uweze kutatuliwa haraka.

ABDU MTULLYA