1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SUFFOLK:Bata mzinga laki moja na alfu 60 waangamizwa nchini Uingereza

5 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUv

Zoezi la kuangamiza bata zaidi ya laki moja na alfu 60 limeendelea nchini Uingereza kwa lengo la kuzuia kuenea ugonjwa wa homa ya ndege. Zoezi hilo lilianza jana kwenye shamba kubwa katika mji wa Suffolk mashariki mwa Uingereza. Wanasayansi wanahofia kuwa aina kali ya ugonjwa huo iliyoua watu zaidi ya 160 katika nchi mbalimbali inaweza kugeuka na kusababisha maambukizi baina ya binadamu kwa urahisi na kwamba mamilioni ya watu wanaweza kufa duniani kote.