1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sunak kuhutubia mkutano mkuu wa Conservative

4 Oktoba 2023

Rishi Sunak anatoa hotuba mchana huu kwenye mkutano mkuu wa chama anachokiongoza cha Conservative unaofanyika huko mjini Manchester akilenga kusafisha haiba ya chama hicho kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

https://p.dw.com/p/4X6Ta
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi SunakPicha: Stefan Rousseau/Pool via REUTERS

Waziri Mkuu huyo anakabiliwa na changamoto kubwa ya kukisafishia njia chama chake kinachokabiliwa na msukusuko kuelekea uchaguzi wa mwaka 2024 baada ya miaka kadhaa ya kashfa na uchumi unaochechemea.

Chama cha Conservative kilicho madarakani tangu mwaka 2010 kinabutura mkia kwenye kura za maoni ya umma nyuma ya chama cha upinzani cha Labour kinachopewa nafasi kubwa ya kurejea madarakani hapo mwakani.

Sunak ataitumia hotuba yake kutangaza mikakati kadhaa anayoamini itaijenga taswira yake kama kiongzi mkakamavu mbele ya wapiga kura waliofadhaishwa na kupanda kwa gharama za maisha ikiwemo nishati ya umeme.