1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yashikilia mpango wa kuwapeleka wakimbizi Rwanda

Lilian Mtono
22 Aprili 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ameahidi hii leo kuanza kuwapeleka Rwanda waomba hifadhi nchini humo miezi michache ijayo.

https://p.dw.com/p/4f3qk
Uingereza | Rishi Sunak
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi SunakPicha: Toby Melville/AP Photo/picture alliance

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ameahidi hii leo kuanza kuwapeleka Rwanda waomba hifadhi nchini humo miezi michache ijayo, kama sehemu ya mpango wa kudhibiti wahamiaji wanaoingia nchini humo ambao hata hivyo umeibua mkanganyiko mkubwa.

Ameuambia mkutano wa waandishi wa habari katika ofisi zake za Downing Street masaa kadhaa kabla ya bunge halijaanza mchakato wa kuidhinisha kipengele muhimu cha pendekezo hilo.

"Waziri Mkuu wa Uingereza: Wiki chache zijazo tutaanza kuchukua hatua. Na kwa kuwa ninajua watu wanataka matendo sio maneno, sitaelezea kwa sasa ni nini hasa kitafanyika na lini. Kuna wachache wenye sauti kubwa ambao watafanya lolote kuharibu mpango wetu. Kwa hivyo hatutatoa maelezo nyeti ya kiutendaji ambayo yanaweza kuzuia hatua zilizofikiwa hadi sasa. Ndege ya kwanza itaondoka baada ya wiki 10 hadi 12."

Baada ya muswada huo kukabiliwa na upinzani mkali baada ya baraza la juu la bunge la Uingereza - House of Lords - kuishinda serikali likishinikiza ulinzi ili kulinda haki za waomba hifadhi, Sunak amesema hii leo serikali itawalazimisha kukaa hadi usiku wa manane hadi utakapopitishwa.