1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Super Tuesday

Kastan, Klaus, Washington (BR)6 Februari 2008

Bado hakuna mshindi aliyejitokeza kati ya wagombea wawili wa Democratics,Hilary Clinton na Barack Obama, licha ya kinyang'anyiro katika majimbno 24 ya Marekani

https://p.dw.com/p/D3Ht
Wafuasi washangiriaPicha: AP


Kinyang'anyiro cha kuania tikiti ya vyama vya Democrats na Republicans ili kugombea wadhifa wa rais wa Marekani kinaendelea kuwasisimua wamarekani na walimwengu kwa jumla.Katika wakati ambapo katika upande wa Republican John McCain anajitokeza kupata imani kubwa ya wafuasi wa chama chake,kwa upande wa wademocrats,bado hakuna hata mmoja,kati ya Hilary Clinton na Barack Obama,anaeweza kudai ameibuka na ushindi baada ya upigaji kura katika majimbo 24 jana jumanne -utaratibu unaojulikana kama "Super Tuesday."
Takriban kura zilizopigwa jumanne ya jana "Super Tuesday" kutoka majimbo yote 24, zimeshahesabiwa -hata hivyo hakuna yeyote kati ya wagombea wawili wa chama cha Democratic aliyeibuka na ushindi bayana:Hilary Clinton na Barack Obama bado wanashindana-idadi ya kura zao takriban zinalingana.Hilary Clinton ameibuka na ushindi katika majimbo makubwa mfano Kalifornia,New-Jersey na New-York.Kwa upande wake Barack Obama ameshinda kama ilivyotarajiwa katika majimbo ya kusini wanakoishi wamarekani wengi weusi.Amejinyakulia ushindi katika majimbo 12 kati ya 21.Kisicho bayana hadi wakati huu,na hali hii inatokana na utaratibu mgumu wa upigaji kura wa chama cha Democratic,ni nani kati ya wagombea hao wawili aliyejikingia kura nyingi zaidi za wajumbe.
Hali bayana zaidi imejitokeza upande wa chama cha Republican:John McCain anaendelea kuongoza.Ingawa Mitt Romney na Mike Huckabee wameshinda katika jumla ya majimbo 11,lakini wako nyuma,mtu akitilia maanani idadi ya kura za wajumbe walizojikingia.McCain ameshinda zaidi Karlifonia na New-York -kwa namna hiyo mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 71 amejikingia sauti za wajumbe wote wa majimbo hayo makubwa.
Ni dhahiri kwa hivyo kwamba jana usiku aliyeshangirwa kua mshindi ni McCain.
"Leo hii tunaweza kudhibitisha,kwamba katika chama cha Republican ,sisi ndio tunao ongoza."
Hilary Clinton na Barack Obama nao pia wameshangiriwa na wafuasi wao.
Shangwe na furaha zilihanikiza kwa namna ambayo hapo awali Hilary Clinton alionekana kutopata nafasi ya kuhutubia.Lakini baadae Senetor huyo wa New York alipata fursa ya kuwaambia wafuasi wake kile ambacho walitaka kukisikia:
"Mko tayari kumchagua rais atakaezifikisha ikulu ya Marekani ,sauti zenu,maadili yenu na ndoto zenu".
Matumaini kama hayo yametolewa pia na Barack Obama katika jimbo lake la Chicago-ingawa hakufikiria kama angeshindwa katika jimbo muhimu la Karlifonia.Obama anasema:
"Kuna kitu ambacho ni muhimu zaidi katika siku hii ya leo ya February,kuliko matokeo ya mwisho:tunatambua wakati wetu umewadia."
Wote wawili Hilary Clinton na Barack Obama wametambua mnamo siku hii ya Super Tuesday-hakuna aliyeibuka na ushindi, upande wa chama cha Democratic-kampeni ya uchaguzi inaendelea.Jumamosi ijayo katika majimbo ya Nebraska na Washington na wiki ijayo katika jimbo la Maryland.


LINK: http://www.dw-world.de/dw/article/0,,3110879,00.html