1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SUVA : Rais avunja bunge na aridhia jeshi kumuondowa waziri mkuu

5 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmV

Rais wa kisiwa cha Fiji leo amelivunja bunge na kuidhinisha jeshi kumuondowa madarakani Waziri Mkuu Laisenia Qarase.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa New Zealand Helen Clark ambaye mara moja ameamuwa kuliwekea vikwazo jeshi la nchi hiyo.

Qarase ambaye amejifungia nyumbani kwake katika mji mkuu wa Suva amesema jeshi linafanya mapinduzi na kwamba hatojiuzulu bali itabidi aondolewe madarakani kwa nguvu.

Qarase ameliambia shirika la habari la Uingereza Reuters kwamba haendi kokote na kwamba yeye ni waziri mkuu aliechaguliwa kidemokrasia wa wananchi wa Fiji na itabidi wamuondowe kwa kutumia nguvu.

Mkuu wa majeshi Frank Bainimarama ametishia mara kadhaa kuipinduwa serikali ya Qarase na kuipa masharti kadhaa ya kujisafisha.Wanajeshi wamezingira makao makuu ya Qarase kuanzia hapo jana.

Kisiwa cha Fiji kimekabiliwa na mapinduzi mara tatu tokea mwaka 1997.