1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SWAT : Wanamgambo wateka vituo 2 vya polisi Pakistan

3 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7AL

Wanamgambo wamesema leo hii wameviteka vituo viwili vya polisi katika eneo la milimani kaskazini magharibi ya Pakistan ambalo limezidi kuwa chini ya udhibiti wa wanamgambo wa siasa kali wenye mafungamano na makundi ya Taliban la Al Qaeda na hiyo kusababisha karaha nyengine kwa serikali ya Rais Generali Pervez Musharraf inayopigwa vita.

Bendera ya wanamgambo hao imepandishwa kwenye mojawapo ya jengo la polisi lililotelekezwa na maafisa wa polisi katika bonde la Swat eneo ambalo limekumbwa na mapigano makali kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo.Masaa machache baadae kituo cha polisi kilioko kilomita 10 kutoka hapo nacho kilitekwa.

Serikali hakitowa taarifa yoyote kuzungumzia madai hayo.