1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sweden, Ukraine zatinga Euro 2016

18 Novemba 2015

Timu za taifa za Sweden na Ukraine ndizo timu za mwisho zilizojikatia tikiti ya kucheza katika dimba la mataifa ya UIaya – UEFA Euro 2016 nchini Ufaransa. Dimba hilo litazijumuisha timu 24

https://p.dw.com/p/1H7kG
EURO 2016 Qualifikation Schweden Dänemark
Picha: Getty Images/AFP/J. Nackstrand

Sweden ilitoka sare ya magoli 2-2 ugenini dhidi ya Denmark, na hivyo wakafanikiwa kufuzu baada ya kuushinda mchezo wa kwanza kwa mabao 2-0.

Mshambuliaji nyota Zlatan Ibrahimovic ndiye aliyefunga mabao yote mawili ya Sweden wakati ya Denmark, yakifungwa na Yussuf Poulsen na Jannik Vestergaard. Ukraine ilijikatia tikiti licha ya kutoka sare ya bao 1-1 na Slovenia. Katika mchezo wa kwanza Ukraine iliishinda Slovenia mabao 2-1.

Timu 24 zilizofuzu kushiriki michuano hiyo ya Ulaya kando na wenyeji Ufaransa ni:

Albania, Austria, Belgium, Croatia, Jamhuri ya Czech, England, Ufaransa, Ujerumani, Hungary, Iceland, Italia, Ireland ya Kaskazini, Poland, Ureno, Jamhuri ya Ireland, Romania, Urusi, Slovakia, Uhispania, Sweden, Uswisi, Uturuki, Ukraine, Wales

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Abdulrahman