1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sweden yatangaza kusisitsha makubaliano na Sweden

Admin.WagnerD11 Machi 2015

Sweden itisitisha makubaliano yake na Saudi Arabia ya thamani ya mabilioni ya fedha katika sekta ya ulinzi, baada ya ukosoaji wake dhidi ya rikodi ya haki za binaadamu ya serikali ya Saudia, kuzua mzozo wa kidiplomasia.

https://p.dw.com/p/1EoYQ
Ägypten Treffen der Außenminister der Arabischen Liga in Kairo
Mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa mjini CairoPicha: Reuters/M. Abd El Ghany

Chama chenye kuongoza serikali ya Sweden, cha Social Democrat, ambacho kiliingia madarakani mwezi Oktoba mwaka jana, kimetoa kipaumbele chake katika sera yake ya mambo ya nje katika suala la haki za binaadamu. Lakini zingatio zaidi likiwa katika uzalishaji viwandani.

Sweden ni taifa lenye kushika nafasi ya 12 duniani katika biashara ya silaha na serikali ya muungano yenye kuliongoza taifa hilo imegawanyika katika suala la kuupitia na kuanzisha upya mkataba wake na Saudi Arabia au la.

Gazeti moja mjini Kiev, Ukraine Dagens Nyheter lilimnukuu Waziri Mkuu Stefan Lofven akisema uamuzi wa makubaliano ya Saudi Arabia yamefanyika kipindi kirefu kilichopita na kwamba kinachofanyika kwa hivi sasa hakijatolewa maamuzi.

Saudi-Arabien Rede König Salman ibn Abd al-Aziz
Mfalme Salman ibn Abd al-Aziz wa Saudi ArabiaPicha: picture-alliance/AP Photo/SPA

Jumatatu hii, Saudi Arabia ilimzuia Waziri wa mambo ya nje wa Sweden, Margot Wallstrom kuhutubia kwenye kikao cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu mjini Cairo, na baadaye jumuiya hiyo ikakubaliana na azimio la kulaani kauli zake, dhidi ya utawala wa Saudia.

Msemaji wa Wallstrom alisema uamuzi huo ulizusha hali ya ukosoaji mkubwa nchini Swden na hasa sauti zikitolewa na wanaharakati wa haki za binaadamu.

Mnamo mwezi Februari, Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden, Margot Wallstrom, aliliambia bunge la nchi yake kwamba Saudi Arabia inavunja haki za wanawake, na akakosoa adhabu ya kupigwa viboko, dhidi ya mwanaharakati wa haki za binaadamu na mwanablogu, Raif Badawi. Waziri huyo pia aliita Saudi Arabia kuwa ni nchi ya kidikteta

Makubaliano hayo ambayo yameelezwa kusitishwa na kughalimu kiasi cha dola bilioni 561 katika kipindi cha mwaka 2011 hadi 2014, yanajumuisha masula ya mifumo ya kijeshi na kuiwezesha Saudia Arabia kiteknolojia.

Rekodi zinaonesha kuwa makubaliano hayo yaliridhiwa kwa mara ya kwanza 2005 na serikali ya awali ya Social Democrat na baadae ukarefushwa tena na serikali ya mrengo wa kati, wa kulia mwaka 2010.

Chama kingine kidogo, chenye kuuna serikali ya sasa kimetaka mkataba huku kufutiliwa mbali kabisa. Lakini wenye viwanda nchini humo wamekuwa wakifanya jitihada za kuurefusha kwa madai ya taifa litapoteza mshirika wake katika sekta ya biashara. Wanadai kusitisha hakutaathiri tu sekta ya kijeshi lakini pia katika maeneo mengine.

Katika barua yao ya wazi walioitoa Ijumaa iliyopita viongozi hao 31 wamesema miongoni mwa waathirika itahusisha tasnia ya mitindo, kwa kutaja uzalisha wa kampuni ya mavazi na yenye maduka makubwa duniani ya H&M.

Mwandishi: Sudi Mnette/RTR
Mhriri: Yusuf Saumu