1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SYDNEY: Korea Kaskazini ingali katika orodha ya ugaidi

4 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSo

Mpatanishi mkuu wa Marekani katika majadiliano yanayohusika na mradi wa silaha za nyuklia wa Korea Kaskazini amekanusha madai ya Pyongyang kuwa Washington imekubali kuiondoa nchi hiyo kutoka orodha ya mataifa yanayotuhumiwa kusaidia ugaidi.

Christopher Hill alipozungumza mjini Sydney alisema,kuondoshwa kutoka orodha hiyo hutegemea hatua zaidi zitakazochukuliwa na Korea Kaskazini kusitisha harakati zake za nyuklia.Hill,mwishoni mwa juma lililopita alikutana na Naibu-Waziri wa Nje wa Korea Kaskazini,Kim Kye Gwan katika mji wa Geneva nchini Uswissi.