1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SYDNEY: Mkutano wa kimataifa kuhusu ukimwi wamalizika

25 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfW

Mkutano wa kimataifa kuhusu ukimwi umemalizika leo mjini Sydney Australia. Mwito umetolewa dawa zinazolenga watoto zitengezwe ili kuhakikisha watoto wanaishi kufukia utu uzima na bila athari zinazotokana na matibabu wanayoyapata.

Watoto takriban milioni 2,3 wameambukizwa virusi vya ukimwi duniani, huku watoto kaisi ya laki sita wakiambukizwa virusi kila mwaka.

Bila matibabu nusu ya watoto walio na virusi vya ukimwi hufariki kabla kufikia umri wa miaka miwili.