1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SYDNEY:Bei ya Koran ni dola milioni 8 na laki nne

19 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqW

Mtawala wa Brunei nchi yenye utajiri mkubwa wa mafuta kusini mashariki mwa Asia amesema kuwa yeye yupo juu ya sheria na kwamba hawezi kushtakiwa kwa sababu ya kughairi mapatano aliyofikia na kampuni moja ya kununua nakala ya kale ya Koran tukufu kwa dola milioni 8 na laki nne.

Gazeti la Daily Telegraph limeripoti kwamba mtawala huyo, sultan Haji Hassanal Bolkiah amejiweka katika kundi la wafalme ambao hawana lazima ya kujibu mashtaka ya mahakama.

Wakili wake ameiambia mahakama kuu ya Australia kwamba sultan hafanyi makosa, ama hakuna makosa yanayofanyika kwa niaba yake.

Kampuni inayoitwa Garsec inakusudia kumshtaki sultani huyo kwa sababu ya kubadili nia, baada ya kukubali kununua nakala hiyo ya Koran miaka miwili iliyopita.