1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SYDNEY:Wakimbizi wa Afrika wapigwa marufuku mpaka Julai ifuatayo

3 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKb

Nchi ya Australia inatangaza kuwa haitakubali tena wakimbizi kutoka bara la Afrika mpaka ifikapo katikati ya mwaka ujao.Hayo ni kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Australia John Howard .Kiongozi huyo anakanusha madai ya ubaguzi wa rangi kwani Australia imekubali wakimbizi alfu 13 kwa mwaka kutoka Afrika ila sasa haja ipo zaidi katika mataifa ya Mashariki ya kati na Asia ili kusawazisha hali hiyo.

Bwana Howard alisema kuwa wakati mwengine inakuwa vigumu kwa wakimbizi kuishi katika jamii za Australia.Waziri wa uhamiaji kwa upande wake Kevin Andrews aliongeza kuwa hata baada ya mwezi Julai mwaka ujao hakuna hakikisho lolote kuwa idadi ya wakimbizi kutoka bara la Afrika itaongezwa.Uamuzi huo unaonyesha hali ilivyobadilika tangu miaka miwili iliyopita wakazi asilimia 70 ya wakimbizi walitoka barani Afrika.

Makundi ya kutetea haki za wakimbizi yanalaumu serikali kwa kukita katika suala hilo huku uchaguzi ukisubiriwa mwishoni mwa mwezi ujao.Chama tawala hakitarajiwi kushinda.