1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria iache kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji

Martin,Prema/ZPR17 Novemba 2011

Umoja wa nchi za kiarabu umetoa muda wa siku tatu kwa serikali ya Syria kusita kutumia mabavu dhidi ya watu wanaoandamana kwa amani na pia kuwaruhusu waangalizi wa kiarabu nchini humo.

https://p.dw.com/p/Rwvd
Kuwaiti foreign minister Mohammed al Sabah, right, Iraqi foreign minister Hoshyar Zebari, center left, Libyan foreign minister Moussa Koussa, center right and Bahrain foreign minster Sheik Khalid bin Ahmed Al Khalifa, right talk while leaving after attending an Arab League Foreign Ministers meeting in preparation for the upcoming Arab League Summit in Sirte, Libya Thursday, March 25, 2010. (AP Photo/Nasser Nasse
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Kiarabu waishinikiza Syria kuacha kutumia mabavuPicha: AP

Syria, imeonywa na umoja huo kuwa itawekewa vikwazo vya kiuchumi, isipochukua hatua hizo. Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za kiarabu mjini Rabat, Morocco umethibitisha kuwa Syria imetengwa kutoka kundi hilo la kiarabu, kwa muda usiojulikana.

Hatua zinazozidi kuitenga serikali ya Rais wa Syria Bashar al-Assad, zimewapa moyo wanajeshi wa Syria walioasi. Imeripotiwa kuwa wanajeshi hao wameshambulia jengo la ofisi ya idara ya upelelezi, ya jeshi la anga mjini Harasta nje ya mji mkuu Damascus. Vile vile wamekishambulia kituo kimoja cha ukaguzi wilayani Hama. Waasi wa kundi linaloitwa jeshi huru la Syria, wamelichagua baraza la kijeshi kwa azma ya kumpindua Rais Assad.