1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria kufaidika na mkutano wa amani ya mashariki ya kati

Abou Liongo26 Septemba 2007

Kushiriki kwa Syria katika mkutano wa kimataifa uliyoitishwa na Marekani juu ya amani ya Mashariki ya Kati, huenda kukaisaidia nchi hiyo kupunguza uhusiano mbaya iliyonayo na jumuiya ya kimataifa.

https://p.dw.com/p/CH7i

Wanadiplomasia hata hivyo wanahisi kuwa itakuwa vigumu kwa nchi hiyo kuondoa baadhi ya matakwa yake kwenye suluhisho la amani ya mashariki ya kati kati ya Israel na Palestina.

Akizungumza mwanzoni mwa wiki hii, Waziri wa Habari wa Syria Mohsen Bilal alisema kuwa nchi hiyo itaamua iwapo itashiriki kwenye mkutano baada ya kupoakea mwaliko.

Amesema kuwa mkutano huo ni lazima ulenge zaidi kutafuta amani ya kwelia kama vile kunazishwa kwa taifa la Palestina, haki ya kurudi kwao wakimbizi wa kipalestina pamoja na kujeshwa Syria kwa milima ya Golan iliyotekwa na Israel.

Waziri huyo ameonya kuwa Marekani na Israel zitafanya kosa kubwa iwapo katika mkutano huo zitachukulia uhusiano kati ya Israel na Syria jambo la kawaida.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Condoleza alisema kuwa nchi hiyo inapanga kualika Syria kwenye mkutano huo unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba, nchini Marekani.

Mwanadiplomasia mmoja wa ngazi ya juu wa Marekani alisema kuwa nchi hiyo inatambua umuhimu wa Syria kuwepo kwenye mkutano huo.

Mwanadiplomasia huyo ambaye alikataa kutaja jina lake amesema kuwa Syria ambayo inawahifadhi mamia kwa maelfu ya wakimbizi wa kipalestina itawajibika kuwa sehemu ya makubaliano yoyote yatakayofikiwa.

Kwa kufanya hivyo itajiondoa katika kutengwa na nchi za Ulaya, Marekani na baadhi ya nchi za kiarabu kwa sababu zinaituhumu kuendesha ugaidi katika nchi za Lebanon na Iraq.

Syria inaliunga mkono kundi la Hamas huko Palestina ambalo hata hivyo haliungwi mkono na nchi za magharibi zikiongozwa na Marekani.Hamas ndiyo walishinda katika uchaguzi wa serikali ya Palestina lakini limetengwa kutokana na kutoitambua Israel.

Rais wa mamlaka ya Palestina Mahamoud Abbas wa chama cha Fath amekuwa akiungwa mkono na Marekani, ambapo akilihutubia Baraza Kuu wa Umoja wa Mataifa Rais George Bush alitaka jumuiya ya kimataifa kumuunga mkono.

OTON:BUSH

Syria imesisitiza kuwa haitakuwa tayari kushiriki kwenye mkutano huo iwapo kutakuwa na ajenda moja ya mpango wa amani kati ya Israel na Palestina.

Maafisa wanasema kuwa nchi hiyo inahitaji mkutano utakaotoa nafasi sawa na wenye uadilifu.

Syria imekuwa ikidai kurejeshewa milima ya Golan iliyotekwa na Israel katika vita vya mwaka 1967 ambapo Israel ikaongeza tena kuteka baadhi ya shemu mwaka 1981.

Majadiliano kati nchi hizo mbili juu ya mzozo huo yalivunjika mwaka 2000, na hali ya uhasama kati ya nchi hizo mbili imeongezeka zaidi toka shambulizi la anga la Israel katika eneo la Syria mwanzoni mwa mwezi huu.

Syria imepeleka malalamiko yake rasmi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya shambulizi hilo.

Vyombo vya habari vya magharibi vimesema kuwa shambulizi hilo lilikuwa ni la kuharibu malighafi ya nuklia ambayo nchi hiyo imeuziwa na Korea Kaskazini.

Lakini Korea Kaskazini na Syria zimekanusha juu ya kuwepo kwa malighafi hiyo.

Hata hivyo Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert alisema kuwa nchi yake haina nia ya kuingia vitani na Syria na kuelezea matumaini yake kuwa hali hiyo ya uhasama iliyojitokeza itamalizika

Israel kwa upande wake haijatoa masharti yoyote ya kushiriki kwenye mkutano huo ikisisitiza kuwa Marekani ndiyo yenye jukumu la kuamua nani wa kumualika.

Msemaji wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo,Ehud Olmert , Miri Eisin amesema kuwa Israel haina tatizo kukaa meza moja na hasimu wake huyo Syria kwenye mkutano huo