1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria: Makamu wa rais hajafikiria kujiuzulu

19 Agosti 2012

Syria imepuuzilia mbali ripoti kuwa Makamu wa Rais Bashar al-Assad amejiondoa serikalini, wakati wanajeshi wake wakifanya mashambulizi dhidi ya waasi katika miji ya Damascus na Aleppo.

https://p.dw.com/p/15sUP
epa02798789 A handout image made available by Syrian news agency SANA showing Syrian vice-president Farouq El Sharea (front centre) heading the meeting of national dialogue staff in Damascus, Syria, 27 June 2011. Meanwhile, more than 190 independent Syrian opposition figures met in Damascus 27 June to discuss ways of ending the government_s violent crackdown on the country's popular uprising. The opposition meeting, the first in Syria since the protests began, was held at a hotel under tight security and in the presence of intelligence services. EPA/SANA/HANDOUT HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES +++(c) dpa - Bildfunk+++
Syrien Farouq El Sharea Dialog in DamaskusPicha: picture-alliance/dpa

Taarifa kutoka ofisi yake imesema kuwa Makamu wa Rais Farouq al-Shara “hajawahi kwa wakati mmoja kufikiria kuondoka nchini humo”. Taarifa hiyo ilirushwa kwenye televisheni ya taifa baada ya kutokea ripoti kuwa mwanachama huyo wa mtiifu wa chama cha Baath alijaribu kujiuzulu na kutorokea Jordan.

Assad, anayekabiliana na uasi uliodumu miezi 17 unaoongozwa na Waislamu walio wengi nchini Syiria wa madhehebu ya Sunni, ametelekezwa na baadhi ya maafisa wakuu serikalini, akiwemo Waziri Mkuu Riyadh Hijab wiki mbili zilizopita.

Baadhi ya viongozi wakuu katika serikali ya Assad wamejiondoa
Baadhi ya viongozi wakuu katika serikali ya Assad wamejiondoaPicha: picture alliance/dpa

Shara, ambaye binamu yake aliye afisa wa ujasusi, alitangaza kujiondoa kwake serikalini yeye binafsi siku ya Alhamisi, ni Muislamu wa madhehebu ya Sunni kutoka mkoa wa Deraa ambako uasi huo ulianzia dhidi ya Assad, ambaye ni mmoja wa kundi la Alawite walio wachache, na ambalo linatokana na Waislamu wa madhehebu ya Shia.

Waziri huyo wa zamani wa Mambo ya kigeni alikuwa mtulivu sana wakati uasi huo ulipoanza lakini akajitokeza hadharani mwezi uliopita katika mazishi ya maafisa watatu wa usalama wa ngazi ya juu katika serikali ya Assad waliouawa katika shambulizi la bomu mjini Damascus.

Taarifa ilisema alifanya kazi tangu kuanza vuguvugu la maandamano ili kutafuta ufumbuzi wa kisiasa wa amani na akaukaribisha uteuzi wa Lakhdar Brahimi kama mpatanishi mpya wa kimataifa kuhusu mzozo wa Syria.

Brahimi ambaye alisita kwa siku kadhaa kabla ya kuikubali kazi hiyo ambayo Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa Gerard Araud aliitajan kuwa ni “ujumbe usiowezekana”, amechukua mahali pa aliyekuwa Katibu Mkuu Kofi Anan ambaye anaondoka mwishoni mwa mwezi huu.

Baadhi ya viongozi wakuu katika serikali ya Assad wamejiondoa
Baadhi ya viongozi wakuu katika serikali ya Assad wamejiondoaPicha: picture alliance/dpa

Mpango wa Annan wenye vifungu sita wa kusitisha machafuko na kuweka njia ya kuwepo mazungumzo ya kisiasa ulizingatia makubaliano ya kuweka chini silaha ya mwezi Aprili ambayo hayakufaulu. Mzozo huo tangu hapo umeendelea kuwa mbaya huku pande zote mbili zikiimarisha mashambulizi yake.

Vikosi vya Assad vimeamua kutumia mashambulizi ya angani ili kuwadhibiti kwa kiasi Fulani waasi walio na silaha katika mji mkuu Damascus na Aleppo, kitovu cha kibiashara upande wa kaskazini. Ziadi ya watu 18,000 wamekufa katika umwagaji damu huo na wengine takribani 170,000 kutoroka nchi hiyo kulingana na Umoja wa Mataifa.

Brahimi atakuwa na wadhifa mpya, Mwakilishi Maalum wa Pamoja kuhusu Syria. Wajumbe wamesema hii ni kumweka mbali na Annan, ambaye alilalamika kuwa mpango wake wa amani uliathiriwa na migawanyiko baina ya nchi za Magharibi zinazomtaka Assad aondoke, na Urusi, ambayo ni mshirika wake muhimu, - katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mwandishi: Bruce Amani/Reuters

Mhariri. Sekione Kitojo