1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria ufunguo kwa suluhisho la Mashariki ya Kati

U.Leidholdt - (P.Martin)25 Februari 2009

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya,Javier Solana amekutana na Rais wa Syria Bashar al-Assad na Waziri wa Mambo ya Nje Walid al-Mualiim mjini Damascus akiwa katika ziara ya juma moja katika Mashariki ya Kati.

https://p.dw.com/p/H1A9
Syrian President Bashar Assad briefs reporters on the outcome of the four-way summit with his French counterpart Nicholas Sarkozy, Emir of Qatar Sheikh Hamad Bin Khalifa al Thani and the Turkish Prime Minister Recep Tayyip Erdogan, in Damascus, Syria, 04 September 2008. Syrian President Bashar al-Assad, hosting a summit of French, Qatari and Turkish leaders, said on 04 September he hoped for direct negotiations with Israel. At the same time, he criticized Israel for not taking part in indirect talks which had been planned for last week in Turkey, which has been mediating between the two sides. EPA/YOUSSEF BADAWI +++(c) dpa - Bildfunk+++
Rais wa Syria Bashar al-Assad.Picha: AP

Kwa maoni ya Marekani na Umoja wa Ulaya, Syria iwe na dhima mpya kusaidia katika kanda hiyo ya Mashariki ya Kati. Sasa mtazamo huo mpya wa kidplomasia kuelekea Syria unapewa msukumo.Syria ilianza kufunguliwa mlango Julai mwaka jana,rais wa nchi hiyo Bashar al-Assad alipoalikwa Paris na Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy.Muda mfupi baadae Sarkozy nae akamtembelea al-Assad mjini Damascus.Baada ya ziara hizo,kila mmoja alingojea serikali kubadilika nchini Marekani.

Tangu Barack Obama kuingia madarakani,wabunge watatu wa Kimarekani wameizuru Syria.Na sasa mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Javier Solana amekwenda Syria. Huko ndio kwenye ufumbuzi wa matatizo mengi ya Mashariki ya Kati.Hata Seneta John Kerry wa Marekani,aliekuwa pia mgeni wa al-Assad hivi karibuni amesema:

"Si siri kuwa baadhi yetu tulikuwa hatukubaliani na sera za serikali yetu ya zamani.Sasa Marekani ikiwa na Rais Barack Obama,serikali mpya na bunge linalodhibitiwa na Demokrats, tuna fursa ya kufuata njia mpya."

Ni matumaini ya Wasyria waliochoshwa kutengwa na kulaaniwa kuwa sasa,watakaribishwa katika jumuiya ya kimataifa.Wakati huo huo,Rais al-Assad anajaribu kusonga mbele kwa kurekebisha uhusiano wake na jirani Libanon na kuzungumza na Israel kupitia upatanishi wa Uturuki.Syria inataka kupata maendeleo katika mazungumzo hayo lakini vile vile inataka irejeshewe Milima ya Golan iliyokaliwa na Israel.

Lakini kuna masuala mengine pia yanayokwamisha kurekebisha uhusiano wake na nchi za magharibi - yaani Syria kuunga mkono makundi ya Hezbollah na Hamas yaliyoorodheshwa na nchi za magharibi miongoni mwa makundi ya kigaidi; ushirikiano wake na Iran na pia kushukiwa kuhusika na mauaji ya Rafik Hariri aliekuwa rais wa Libanon.

Rais wa zamani wa Marekani George W.Bush,alitumia vikwazo na vitisho kuishinikiza Syria bila ya kufanikiwa. Sasa,Barack Obama anafuata sera za maafikiano kutenzua matatizo. Syria imepewa dhima muhimu huku Seneta Kerry akifanya mazungumzo na nchi yenye uhusiano wa shida na Marekani lakini,ni ufunguo kwa suluhisho la Mashariki ya Kati.