1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SYRIA: vita vya wenyewe kwa wenyewe vyanukia

27 Mei 2012

Mkuu wa ujumbe wa umoja wa mataifa ameonya kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe Syria baada ya wachunguzi hao kuhesabu miili 92, 32 ikiwa ni ya watoto ,katikati ya mji wa Houla kufuatia ripoti za mauaji.

https://p.dw.com/p/1535z
The bodies of people whom anti-government protesters say were killed by government security forces lie on the ground in Huola, near Homs May 26, 2012. The death toll has risen to at least 90 from Syrian shelling on the town of Houla on Friday, an opposition group said on Saturday. The UK-based Syrian Observatory for Human Rights said residents continued to flee the town, in central Homs province, in fear that artillery fire would resume. REUTERS/Shaam News Network/Handout (SYRIA - Tags: CIVIL UNREST) FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. THIS IMAGE HAS BEEN SUPPLIED BY A THIRD PARTY. IT IS DISTRIBUTED, EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS
Miili ya watoto na watu wazima ikiwa imepangwa mjini Huola, nchini SyriaPicha: Reuters

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amejiunga na sauti za kimataifa kushutumu mauaji hayo siku ya Jumamosi , huku kukiwa na miito kwa dunia kuchukua hatua kusitisha umwagikaji wa damu.

U.N.-Arab League envoy Kofi Annan speaks during a news conference at Hatay airport, southern Turkey, April 10, 2012. Annan said there should be no preconditions to halting violence in Syria and insisted a U.N.-sponsored peace plan designed to stem 13-months of conflict was still on the table. Speaking just hours before the end-of-day deadline for Syria to implement the ceasefire plan, Annan said Syrian forces had withdrawn from some areas but moved to others not previously targeted, and the situation was not as he had hoped. REUTERS/Stringer (TURKEY - Tags: POLITICS CIVIL UNREST SOCIETY IMMIGRATION)
mjumbe wa UN na Arab league nchini Syria Kofi AnnanPicha: Reuters

Jeshi la waasi la Free Syria, Syria huru , FSA, limesema halifuati tena mpango unaoungwa mkono na umoja wa mataifa nchini Syria hadi pale kutakapokuwa na uingilia kati wa umoja wa mataifa kuzuwia mauaji ya raia, na kutoa wito wa mashambulio ya anga dhidi ya majeshi ya serikali.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe

Mkuu wa ujumbe wa umoja wa mataifa meja jenerali Robert Mood amekiita kile kilichotokea mjini Houla , kuwa maafa ya kinyama. Wachunguzi wa kiraia na kijeshi wa Umoja wa mataifa walikwenda mjini Houla na kuhesabu miili 32 ya watoto na zaidi ya 60 ya watu wazima waliouwawa, Mood amewaambia waandishi habari mjini Damascus siku ya Jumamosi.

Norwegian Major-General Robert Mood, chief of the United Nations Supervision Mission in Syria (UNSMIS), speaks to the media at a hotel in Damascus May 16, 2012. REUTERS/Khaled al- Hariri (SYRIA - Tags: CIVIL UNREST POLITICS MILITARY CONFLICT HEADSHOT)
Meja jenerali Robert MoodPicha: REUTERS

Kundi linalochunguza hali nchini Syria limesema kuwa watu 114 wameuwawa katika mji wa Houla. Yeyote alieanzisha, yeyote anayehusika na yeyote aliyefanya vitendo hivyo vya kuchukiza anapaswa kuwajibishwa, amesema Mood.

Wale wanaotumia nguvu kwa ajili ya kutimiza ajenda zao wataleta hali ya kutokuwa thabiti zaidi, hali ambayo haitabiriki na huenda ikaelekeza nchi hiyo katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, ameongeka mkuu huyo wa ujumbe wa umoja wa mataifa.

Ban Ki-moon na Kofi Annan ambaye ni mjumbe wa umoja wa mataifa na mataifa ya umoja wa mataifa ya kiarabu , Arab League, ambaye amekuwa mpatanishi wa makubaliano ya kusitisha mapigano, ambayo yamekuwa yakikiukwa kila siku tangu yalipoanza kufanyakazi Aprili 12, wamesema kuwa mauaji hayo ya kinyama yanakiuka sheria za kimataifa.

Uhalifu huu wa kinyama na unaochukiza , uliowahusisha matumizi bila kujali na ya kupita kiasi ya nguvu , ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa, msemaji wa umoja wa mataifa amemnukuu katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon akisema.

Marekani nayo yashutumu

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton pia ameshutumu vikali , mauaji hayo na kusema Marekani itafanyakazi pamoja na washirika wake wa kimataifa kuongeza mbinyo dhidi ya rais Bashar al-Assad na washirika wake.

Secretary of State Hillary Rodham Clinton speaks during a news conference at the State Department in Washington, Thursday, May 24, 2012, to discuss the State Department's annual report on human rights. (AP Photo/Manuel Balce Ceneta)
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Rodham ClintonPicha: dapd

Utawala unaohusisha mauaji na hofu ili kuwatawala raia wake ni lazima ufikie mwisho, ameongeza. Shutuma pia zimemiminika kutoka umoja wa Ulaya. Uingereza, Ufaransa na Ujerumani , huku waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius akisema kuwa anafanya matayarisho ya mkutano wa marafiki wa Syria.

Mwenzake wa Uingereza William Hague amesema , "tutatoa wito wa kufanyika kioa cha dharura cha baraza la usalama la umoja wa mataifa katika siku za hivi karibuni."

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle amesema ameshtushwa na kuchukizwa na mauaji hayo.

Meja jenerali Mood amethibitisha kuwa makombora na vifaru viliishambulia mji wa Houla na kutoa wito kwa serikali ya Syria kuacha kutumia silaha kali na kwa makundi yote kusitisha matumizi ya nguvu kwa aina yoyote ile iwayo.

Mwandishi : Sekione Kitojo

/ afpe / dpae

Mhariri: Amina Abubakar