1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria yaendelea kutumia nguvu kukandamiza upinzani

Martin,Prema/zpr21 Desemba 2011

Licha ya makubaliano yaliyofikiwa na Umoja wa Nchi za Kiarabu, Syria inaendelea kutumia nguvu dhidi ya wapinzani na wanajeshi wake wanaoasi kwenda kujiunga na upande wa upinzani.

https://p.dw.com/p/13Wpm
In this image from TV shown on the internet made available by the Sham News Network Tuesday Dec. 20, 2011, protesters chant slogans in Homs, Syria. Amateur video emerged on Monday, Dec.19, 2011, from Syria, which purported to show ongoing violence in the restive country. (Foto: Sham News Network, via APTN/AP/dapd) TV OUT THE ASSOCIATED PRESS HAS NO WAY OF INDEPENDENTLY VERIFYING THE CONTENT, LOCATION OR DATE OF THIS VIDEO IMAGE.
Waandamanaji wapinga ukandamizaji unaoendelea SyriaPicha: Sham News Network/dapd

Kituo cha wanaharakati wa haki za binadamu wa Syria mjini London, kimeripoti kuwa wanajeshi 100 walioasi, walizingirwa na waliuawa au walijeruhiwa wilayani Idlib. Siku ya Jumatatu pia wanajeshi 70 walioasi waliuawa katika wilaya hiyo iliyo karibu na mpaka wa Uturuki. Wanaharakati wanasema, hapo jana vile vile raia 33 waliuawa huko Idlib na Homs.
Umoja wa Nchi za Kiarabu umesema, tume ya wajumbe wake kesho inakwenda Syria. Katika makubaliano yaliyopatikana siku ya Jumatatu kati ya umoja huo na Syria, serikali ya Rais Bashar al-Assad imekubali kuacha kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji, kuwaruhusu waangalizi nchini humo na kuyaondoa majeshi yake kutoka maeneo yaliyo ngome za upinzani.