1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Syria: Zaidi ya muongo mmoja wa mateso na mauaji.

Selina Mdemu10 Julai 2023

Serikali ya Syria inayoongozwa na Bashar al Assad imeanza kurejea kwenye mfumo wa kidiplomasia kwa kasi, licha ya kuwa ukiukwaji wa haki za binaadamu na uhalifu unaofanywa na serikali bado unaendelea kama kawaida.

https://p.dw.com/p/4Th0O
Flash-Galerie Unruhen Syrien Jemen
Picha: AP

Licha ya mzozo huo kuelekea ukingoni, lakini kwa upande wa ukiukwaji wa haki za binaadamu, hakuna kilichobadilika. Shirika la Haki za Kibinadamu la Syria lenye makao yake nchini Uingereza katika ripoti yake ya kipindi cha nusu mwaka imeeleza kuwepo kwa jumla ya vifo 501 vitokanavyo na mateso, na waathiriwa zaidi wakiwa ni watoto 71 na wanawake 42.

Fadel Abdul Ghany ambaye  ni mkuu wa Mtandao wa Haki za Kibinadamu wa Syria wenye makao yake nchini Uingereza, SNHR, ameiambia DW kuwa "tabia ya Rais Assad haibadiliki, hajali kuhusu mateso wanayopitia watu wa Syria."

Abdul-Ghany anasema Wasyria wengi wanahisi wanaishi katika hali ya hatari. Kesi mbalimbali zilizoripotiwa na SNHR zinaonesha hali ya hatari, mfano kesi ya kijana Khalif Homsi al-Sayed alieuawa kwa kupigwa risasi katika mji wa Sabikhan, eneo linalodhibitiwa na serikali ya Assad.

Maandamano ya kumpinga Rais Assad 2011
Maandamano ya kumpinga Rais Assad wa Syria mwaka 2011Picha: picture-alliance/dpa

Lakini si serikali ya Syria pekee inayohusika masuala ya uhalifu nchini humo. Kundi hilo la haki za binadamu pia limeripoti matukio mengine ya jinai yanayofanywa na makundi mengine ya wapiganaji Syria. Limetolea mfano wa miaka miwili iliyopita ambapo kijana Abdul Karim Ahmad al-Shabib alitekwa nyara kisha kuuawa kwa kupigwa risasi na kundi la wanamgambo la Hayat Tahrir al-Sham, ambalo linadhibiti sehemu inayoshikiliwa na upinzani nchini Syria.Maandamano makubwa yafanyika Syria

Nayo ofisi ya Mambo ya nje ya Ujerumani hivi karibuni imeelezea hali ya haki za binadamu nchini Syria kuwa ni  "janga." Neno ambalo limetumika katika hati ya ndani iliyooneshwa na shirika la utangazaji la Ujerumani NDR.

Rebekka Rexhausen, ambae ni mtaalamu kutoka Syria anayefanya kazi na shirika la haki za binadamu. ameiambia DW kuwa  "Utafiti waliofanya umeonesha kuwa watu wa Syria waliokimbia wameainishwa kama wapinzani wa Rais Assad au wanachukuliwa kuwa wasaliti, matukio kadhaa yakiwemo "Mashambulio ya mabomu kwenye majengo ya kiraia kama vile hospitali au shule,  watu kutoweka na kukamatwa kiholela, utesaji na hukumu za kifo bila kesi za awali bado ni jambo la kawaida,

Rebekka ameongeza, kusema hii ni sababu kwa nini haiwezekani kuwarudisha wakimbizi. kwa maana yeyote anaebainika kukosoa utawala wa Assad bado yuko hatarini. Lakini hata wenyeji ambao hawajihusishi na siasa wanaishi kwa hofu  ya ukosefu wa usalama,  kwani wanakabiliwa na tishio la kuandikishwa kwa nguvu  katika jeshi la Syria pamoja na mashambulizi yanayoendelea dhidi ya walengwa wa kiraia na mikakati ya serikali ya Assad.Mwaka mmoja wa machafuko nchini Syria

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeandika "ukiukaji wa kutisha'' kufuatia kile wanachokumbana nacho wakimbizi wanaorejea Syria kuwa limeeleza kuwa "Vikosi vya usalama vya Syria vimewaweka kizuizini Wasyria waliorejea nyumbani baada ya kutafuta hifadhi nje ya nchi

 Bashar al Assad
Rais wa Syria Bashar al AssadPicha: picture alliance/dpa

Nae Abdul Ghani ambae ni mwanaharakati wa haki za binadamu ameiambia DW, kuwa kutokujali kwa Assad kunamfanya tu kutaka kuendelea kama ambavyo amekuwa akifanya kwa miaka mingi. Ghani ameelezea  lengo la Assad ni kutaka familia yake iendelee kutawala Syria, kama baba yake alivyofanya kabla yake na, kama anatarajia mwanawe atatawala baada yake.Maandamano makubwa kuitikisa Syria

Mambo haya yote yanatokea wakati ambapo serikali ya Syria kwa zaidi ya muongo mmoja mfumo wake wa kidiplomasia unajaribu kurudi kwenye jukwaa la kimataifa. Licha ya uhalifu wa kivita uliothibitishwa na serikali, mamilioni ya watu waliokimbia makazi yao, takribani nusu milioni ya watu kufa na uwepo vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo havijatatuliwa kwa muda mrefu, Syria imealikwa kurejea kwenye chombo cha ushirikiano wa kikanda wa Jumuiya ya Kiarabu ambao hapo awali ilikuwa imesimamishwa.