1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taasisi za utafiti za Ulaya na Marekani zakata mawasiliano na Taasisi ya taaluma za siasa na uhusiano wa kimataifa huko Iran.

17 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CBHz

Tehran:

Karibu ya taasisi za utafiti 40 za Ulaya na Marekani zimesema zitasimamisha mawasiliano na taasisi maarufu ya utafiti katika Iran ambayo ilisaidia kuandaa nchini humo mkutano wa wiki iliopita uliohudhuriwa na watu wanaokana juu ya kutokea mauaji ya kiholela ya Wayahudi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Taasisi hizo zimekubali kusitisha programu zinazoendelea sasa pamoja na taasisi ya Iran juu ya taaluma za siasa na uhusiano wa kimataifa. Mkutano huo uliofanywa wiki iliopita uliwakusanya watu kutoka sehemu mbali mbali za dunia wanaokana juu ya kutokea mauaji ya kiholela dhidi ya Wayahudi. Watu hao walijadiliana kama mauaji hayo yalifanyika.