1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taipei. China kufitini taiwan na mataifa ya Afrika.

20 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD10

China inampango wa kuanzisha juhudi za kibalozi kuitenga Taiwan katika mkutano kati ya China na mataifa ya Afrika, lakini mataifa matano washirika wa Taiwan yamekataa kuhudhuria mkutano huo.

China imekuwa kila mara ikijaribu kuitenga Taiwan katika mikutano kama hiyo.

China itakuwa mwenyeji wa mkutano wa tano wa kila mwaka kati ya China na mataifa ya Afrika mjini Beijing kuanzia Novemba 2-6 ili kuimarisha mahusiano ya kisiasa na kiuchumi na washirika 46 wa China katika bara la Afrika.