1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taliban wapata kipigo Afghanistan

11 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CaBR

KABUL.Majeshi ya Afghanistan yamefanikiwa kuwafurusha wapiganaji wa Taliban katika ngome yao huko kwenye mji wa kusini wa Musa Qala.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Aghanistan Generali Mohammad Zahir Azimi amesema kuwa vikosi vya serikali sasa vinaudhibiti mji huo lakini wanahisi kuwa huenda wapiganaji wa Taliban wako kwenye viunga vya mji huo wa Musa Qala.

Mafanikio hayo yamekuja mnamo wakati ambapo Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown amefanya ziara ya ghafla nchini Afghanistan ambako kuna vikosi vya Uingereza katika jeshi la NATO.