1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TALLINN:Vurugu zaendelea Estonia

28 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6I

Vurugu zimeendelea katika mji mkuu wa Estonia Tallin kwa siku ya pili, huku Polisi wakilazimika kufyatua risasi za mpira kwa wandamanaji wenye hasira.

Vurugu hizo zinafuatia kuondolewa kwa sanamu ya kumbukumbu ya kivita ya Urusi katika mji mkuu huo.

Hapo jana mtu mmoja aliuawa na wengine zaidi ya 43 kujeruhiwa katika vurugu hizo.

Urusi imesikitishwa na uamuzi wa serikali ya Estonia nchi ambayo ilikuwa katika iliyokuwa shirikisho la sovieti ya zamani.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov amesema kuwa nchi hiyo itachukua hatua kali dhidi ya uamuzi huo, na baraza la shirikisho la Urusi limetaka kuvunjwa kwa uhusiano wa kidiplomasia na nchi hiyo.

Zaidi ya robo ya watu milioni moja na laki tatu nchini humo wana asili ya Urusi.