1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tamasha za kitamaduni - Ruhr 2010

4 Januari 2010

Mwaka 2010 ni mwaka wa msisimko wa kitamaduni kwa eneo la Ruhr nchini Ujerumani licha ya msukosuko wa uchumi.Eneo hilo linaloanzia mji wa Duisburg hadi Dortmund, limepata cheo cha jiji la utamaduni barani Ulaya.

https://p.dw.com/p/LKwD
Deutschland Kulturhauptstadt Ruhrgebiet Ruhr 2010 Logo
Nembo ya RUHR 2010 -mji mkuu wa utamaduni Ujerumani.

Je, Umoja wa Ulaya unaazimia kitu gani kwa kutoa cheo hicho cha jiji la utamaduni? Fikra ya kuwa na jiji la kitamaduni imetoka kwa muimbaji wa zamani Melina Mercouri mwaka 1985 pale alipokuwa waziri wa utamaduni wa Ugiriki. Wakati huo Ugiriki ilishika wadhifa wa urais wa Jumuiya ya Ulaya na ilikuwa ikipitia kipindi kigumu cha kisiasa.

Mercouri alitafuta njia ya kuchangamsha mandhari ya kisiasa kwa kuwa na tamasha mbali mbali za kitamaduni. Hivyo basi muimbaji Mercouri aliufanya mji wa Athens kuwa mji mkuu wa kwanza wa utamaduni.Tamasha hizo za kitamaduni mjini Athens ziliendelea kwa majuma machache tu, wakati wa majira ya joto. Baadae ikafuata miji mingine: Florenz,Amsterdam,Berlin na Paris.

Die griechische Schauspielerin, Sängerin und Politikerin Melina Mercouri mit ihrem Ehemann, dem Regisseur Jules Dassin, während der Berliner Filmfestspiele im Februar 1984. Die griechische Schauspielerin und Kultusministerin Melina Mercouri ist am 6. März 1994 nach langem Leiden in New York gestorben, wohin sie sich zur Behandlung ihres Lungenkrebses begeben hatte. Sie hatte sich in Filmen wie "Sonntags...nie" und "Topkapi" international einen Namen gemacht bevor sie in die Politik ging. Melina Mercouri, eigentlich Maria Amalia Mersuris, wurde am 18. Oktober 1925 in Athen geboren. Schlagworte Personen, Politik, Kultur, Medien, Film, Festspiele, lächeln
Melina Mercouri, waziri wa zamani wa utamaduni wa Ugiriki.Picha: picture-alliance/dpa

Lakini katika mwaka 1990, tamasha hizo zilichukua sura mpya kabisa katika mji wa Glasgow huko Scotland. Tamasha za kitamaduni zilibadilika kuwa maonyesho makubwa ya kitamaduni. Siku hizi, miji inagombea kuchaguliwa, takriban sawa na mashindano ya kutaka kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki.

Katika mwaka 2004 Umoja wa Ulaya ulipata wanachama kumi wapya na sasa kuna jumla ya nchi 27, na kila mwaka si chini ya miji miwili huchaguliwa kama miji mikuu ya utamaduni. John Macdonald wa Halmshauri ya Umoja wa Ulaya mjini Brussles anaeleza:

"Tulitambua mwaka 2004 kuwa baada ya kupata wanachama wapya itachukua muda mrefu mno kuzunguka katika nchi zote wanachama katika Umoja wa Ulaya."

Utafiti uliofanywa na Halmashauri ya Umoja umeonyesha kuwa miji inayopewa hadhi ya miji mikuu ya kitamaduni inafaidika. Mwanahistoria Jürgen Mittag wa taasisi inayoshughulikia masuala ya waanyonge mjini Bochum anasema, tamasha hizo sasa si tena sherehe za kuonyesha utamaduni wa Ulaya, bali zimekuwa biashara kubwa, kwa kiwango ambacho wala kisingedhaniwa katika mwaka 1985. Sasa tamasha hizo za kitamaduni zinavutia eneo zima,sio jiji lililohusika tu.

Kwa mfano, bajeti ya tamasha za Ruhr mwaka 2010 imefikia Euro milioni 65 na fedha hizo zimechangwa na miji ya eneo la Ruhr na wafadhili wa binafsi. Kwa mujibu wa John Macdonald, Umoja wa Ulaya hutoa msaada wa Euro milioni moja na nusu tu. Hata hivyo, miji ya Ulaya imepangana kuwania cheo cha jiji la kitamaduni na hivi sasa zinapaswa kungojea miaka sita kabla ya kujua iwapo zimechaguliwa au la.

Mwandishi:Riegert,Bernd/ZPR/P.Martin

Mhariri: Othman, Miraji