1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania: Chama cha CUF kinataka muwafaka wa Zimbabwe uigwe Zanzibar

Othman, Miraji17 Septemba 2008

Muwafaka wa Zimbabwe uigwe Zanzibar, inasema CUF

https://p.dw.com/p/FJzV
Ripota wa Deutsche Welle, Mohammed Abdul Rahman(kushoto), na mtetezi wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha CUF, Seif Shariff Hamad(katikati), katika kituo cha kupigia kura huko Zanzibar mwaka 2005Picha: Mohamed Abdulrahman/DW

Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Upinzani cha Tanzania, CUF, Profesa Ibrahim Lipumba,ametoa mwito kwa Rais Jakaya Kikwete wa nchi hiyo, ambaye pia ni mweyekiti wa Umoja wa Afrika, AU, aige mfano wa kupatikana muwafaka wa kisiasa baina ya vyama vinavopingana huko Zimbabwe na Kenya na kuwa kichocheo kwake ili upatikane kwa haraka muwafaka wa kisiasa huko Visiwani Zanzibar baina ya chama tawala cha CCM na chama chake cha CUF. Hayo aliyasema katika mahojiano ya simu aliofanyiwa.