1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania: Chiligati azungumza juu ya kashfa za rushwa na Muwafaka wa Zanzibar

Othman, Miraji30 Septemba 2008

Waziri Chiligati wa Tanzania ajibu juu ya madai ya rushwa ndani ya chama tawala na serikalini

https://p.dw.com/p/FR3g
Willy Brandt, kiongozi wa Chama cha SPD katika miaka ya sabini, na ambaye pia aliwahi kuwa kansela wa UjerumaniPicha: AP

Kwa mwaliko wa Wakfu wa Friedrich Ebert ulio karibu na Chama cha Social Democratic, SPD, hapa Ujerumani, katibu wa itikadi wa Chama tawala cha CCM nchini Tanzania, John Zephania Chiligati, ambaye pia ni waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makaazi, amekuweko hapa Ujerumani kwa wiki nzima. Vyama vya SPD na CCM vina urafiki na ushirika wa miaka mingi tangu zama za viongozi wa vyama hivyo, marehemu Willy Brandt na Mwalimu Julius Nyerere. Alipolitembelea jengo letu la Deutsche Welle, nilipata nafasi ya kuzungumza naye, na kwanza niltaka kujuwa zaidi kutoka kwake juu ya madai ya kashfa za rushwa ambazo zimewakumba viongozi kadhaa wa chama na serekali huko Tanzania, jambo ambalo wachunguzi wanasema limekipunguzia umaarufu chama cha CCM....