1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania kuaga miili ya waliofariki katika ajali ya ndege

7 Novemba 2022

Maandalizi ya kuaga miili ya watu 19 waliofariki jana katika ajali ya ndege ya Precision Air katika Ziwa Victoria kufanyika leo Bukoba, Mkoani Kagera.

https://p.dw.com/p/4J8ik
Tansania | Flugzeugabsturz in den Victoriasee
Picha: REUTERS

Maafisa wa serikali walitangaza kwamba watu 19 walikufa baada ya ndege ya abiria ya shirika la ndege za Precision la nchini Tanzania kuanguka katika ziwa Viktoria wakati ikikaribia kutua uwanjani. Afisa mwandamizi wa polisi amesema kulikuwa kunanyesha wakati ndege ilipotumbukia majini. Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa alipandisha idadi ya waliokufa kutoka watatu waliotangazwa awali. Maafisa walisema awali kwamba watu 26 kati ya 43 waliokuwemo kwenye ndege hiyo iliyokuwa inatokea Dar es Salaam kuelekea Bukoba, waliokolewa na kupelekwa hospitali. Haikubainika wazi iwapo idadi mpya ya vifo inahusisha watu waliokufa hospitali.