1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania na Afrika Kusini zakataa kusaini mkataba AU

28 Januari 2013

Afrika Kusini na Tanzania zimekataa kuhusika katika sherehe ya makubaliano ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Nchi hizi zinasema kuwa hazikuarifiwa juu ya jambo hili na hivyo hazitaki kuwa chanzo cha mvutano kandani.

https://p.dw.com/p/17SgR
Heads of the African States pose for a group picture in Addis Ababa, Ethiopia, Sunday, Jan, 27, 2013, during the African Union Conference. African leaders met in the Ethiopian capital Sunday for talks dominated by the conflict in Mali as well as lingering territorial issues between the two Sudans. The African Union says it will deploy a force in Mali, where French troops are helping the Malian army to push back Islamist extremists whose rebellion threatens to divide the West African nation. (Foto:AP/dapd)
Addis Ababa Äthiopien Konferenz Afrikanische UnionPicha: AP

Lakini waziri wa usalama wa Afrika kusini , anasema kuwa kwa mashangao wao walipowasili jijini Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya mkutano wa umoja wa Afrika walipata barua ambayo ilisema kuwa Afrika kusini ilikuwa imekubali kuwa ingekuwa kati ya nchi washahidi wa mipango ambayo inatafuta sulushu nchini Kongo. Waziri wa Usalama Nosiviwe Mapisa anaelezea:

"Hii ilitushangaza kwani hiyo si aina ya mkataba amabyo nchi yeyote inaweza kujihusisha nayo kwa urahisi, kunafaa kuwe na mikutano na majadialiano kwa undani kati yetu kuhakikisha kuwa tuaelewa tunayojihusisha nayo. Labda mkataba amabyo imetengeneza tayari haina shida lakini jinsi jambo hili limejitokeza si mzuri, inaweza kuleta shida sana kati ya nchi zetu."

Mkataba kusainiwa iwapo nchi zote zitahusishwa

Kulingana na hati ambayo ilikuwa tayari imetayarishwa kuhusu swala la Kongo nchi za kutoka jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika, Angola, Afrika Kusini na Tanzania ndizo zingetarajiwa kuwa washahidi kuhusika katika sherehe ya kutia saini makubaliano ya Kongo. Nosiviwe Mapisa waziri wa usalama wa Afrika kusini anaelezea tena.

Waasi wa M23 bado wanatishia amani DRC
Waasi wa M23 bado wanatishia amani DRCPicha: Phil Moore/AFP/Getty Images

"Swali letu ni, kwa nini nchi zingine hazijahusihwa? Kwasababu tumekuwa tukijaribu kutatua swala la Kongo tukiwa nchi 14, kwa hivyo sisi kukubali kuhusika pekee yetu katika shere hii ingefanya kuwe na mvutano usiofaa."

Tanzania na Afrika Kusini zimedhihirisha kwamba zitahusika kutia saini tu katika makubaliana kuhusu Kongo ambayo itahusisha nchi zote zilizohusika katika kutafuta suluhu kwa Kongo yaani nchi wanachama wa maziwa makuu na nchi zote za jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika.

Mwandishi: Coletta Wanjohi/DW Addis Ababa

Mhariri: Mohammed Khelef